Kulingana na ( 1 Petro 4:1) Ni silaha ya nia gani aliyokuwa nayo Kristo ambayo na sisi tunapaswa kujivika? 

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

1 Petro 4:1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, NINYI NANYI JIVIKENI SILAHA YA NIA ILE ILE; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 

JIBU: Silaha ya nia aliyokuwa nayo Kristo ambayo na sisi tunapaswa kujivika, ni  NIA NA KUSUDI la kukubari kutesaka na kufa, kuliko kushindwa kutimiza kusudi la Mungu la yeye kufa msalabani ili watu wa mataifa yote wapate wokovu, hiyo ndio nia iliyokuwa ndani Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, alidhamiria ndani yake kukubali kupitia shida, dhiki na mateso kuliko kushindwa kutimiza kusudi la Mungu la yeye kufa msalabani, sasa hiyo nia aliyokuwa nayo Kristo inafananishwa na sila ambayo na sisi pia tulio mwamini hatuna budi kujivika katika maisha yetu ya wokovu.

Kristo kama njia, alistahimili hayo mateso bila kujali matusi na dhihaka na kuyafanya mapenzi ya Mungu, ili Yeye awe kama kielelezo kwa wale wote watakao mfuata baadaye.

1 Petro 2:21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; MAANA KRISTO NAYE ALITESWA KWA AJILI YENU, AKAWAACHIA KIELELEZO, MFUATE NYAYO ZAKE.

Silaha ya nia hiyo hiyo ilikuwepo pia kwa mitume wa Bwana Yesu, wakifuata kielelezo cha Kristo, walikubali kupigwa na kuteswa ili tu wayafanye mapenzi ya Mungu, watu mbali mbali walio mwamini, walibirutwa magerezani na Sauli lakini walibaki katika kusudi la Mungu kwa silaha ya nia hiyo.

Hivyo na sisi, kama wanafunzi wa Bwana Yesu, hatuna budi kuwa na silaha ya nia hiyo ya kumpenda Mungu bila kujari gharama, ni heri kukubali kutengwa na familia kiliko kukubali kushiriki katika mambo ya uganga na uchawi, ni heri kukosa kazi kuliko kukubali kuvaa mavazi ya kikahaba, ni heri kutengwa na marafiki kuliko kushirikiana nao katika ulevi, disco, uasherati, fashion n.k kwani tukifanya hivyo na kustahimiri hadi mwisho, tutamiliki na Mwokozi Wetu, lakini tukimkana naye atakutana.

2 Timotheo 2:12 KAMA TUKISTAHIMILI, TUTAMILIKI PAMOJA NAYE; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; 

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312MADA ZINGINEZO:

Bado Bwana Yesu anasema nawe kwa mifano?


SABURI NI NINI KATIKA BIBLIA?


Itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni.


Kivipi tunafarakana na imani kwa kutamani fedha?

LEAVE A COMMENT