Mbegu iharibikayo ni ipi? (1 Petro 1:23)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized


1 Petro 1:23  Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa MBEGU IHARIBIKAYO, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 

Mbegu iharibikayo ni ile ya mwili wa damu na nyama, ambayo wanadamu wote tunazaliwa katika hiyo kutoka kwa Adamu wa kwanza. Kila mtu aliyezaliwa kwa mapenzi ya mwili na damu, huyo ni mbegu iharibikayo kwa sababu, kupitia kwa Adamu wa kwanza ndipo uharibifu ulipoingia, yaani ardhi kulaaniwa, na mbaya zaidi mauti


Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 

18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 

19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. 

Lakini Adamu wa pili, yaani Yesu Kristo (1 Wakorintho 15:45-47) yeye sio mbegu iharibikayo tena kama alivyokuwa Adamu wa kwanza, bali ni mbegu ISIYOHARIBIKA (kwani Yeye aliishida mauti), ni mbegu inayodumu milele na milele, na wote wanaozaliwa kwake hawazaliwi kwa mapenzi ya mwili tena kama ilivyokuwa kwa Adamu wa kwanza, bali wanazaliwa upya kwa mapenzi ya Roho na kuwa viumbe vipya.

Yohana 3:6  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na KILICHOZALIWA KWA ROHO ni roho.

 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, HAMBA BUDI KUZALIWA MARA YA PILI. 


Na tena, kama vile Adamu wa kwanza alivyopewa mamlaka ya kutawala juu ya vitu vyote duniani yeye na wazao wake (lakini alianguka katika dhambi) ndivyo ambavyo Adamu wa pili, Yesu Kristo, alivyopewa mamlaka ya kutawala, siyo ya vitu vya duniani tu, bali na vya mbinguni, yeye na uzao wake.

Waebrania 2:8 UMEWEKA VITU VYOTE CHINI YA NYAYO ZAKE. KWA MAANA KATIKA KUWEKA VITU VYOTE CHINI YAKE HAKUSAZA KITU KISICHOWEKWA CHINI YAKE. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake.

9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.

 10 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, AKILETA WANA WENGI WAUFIKILIE UTUKUFU, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 

Sasa ili usiendelee tena kuwa mbegu iharibikayo, na kuwa mbegu isiyoharibika na kutawala na Adamu wa pili, huna budi kuzaliwa upya kwa kumwamini Yesu Kristo kunako ambatana na kutubu dhambi zako, na kisha kubatizwa kwa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina lake, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu atakaye kuwezesha kujifunza maandiko na kukuwezesha kuyafanya mapenzi ya Mungu na kuyatoa matunda yake  ya utakatifu.

Lakini, kama bado hujamwamini Yesu Kristo na kubatizwa kwa jina lake na kupokea Roho wake Mtakatifu ambaye ni muhuri wa Mungu, kamwe hutoweza kuingia katika ufalme wake na kutawala naye.

Yohana 3:5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

 +255652274252/ +255789001312Mada zinginezo:

Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.


Ni hukumu ipi ya Ibilisi inayozungumziwa katika Waraka wa (1 Timotheo 3:6?)


Je! Kuna Mungu wawili? (Kulingana na Yohana 1:1)


UMESHAIFAHAMU NA KUIPOKEA BARAKA YA IBRAHIMU KATIKA MAISHA YAKO .


Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?

LEAVE A COMMENT