AKAIFANYA IWE ISHARA KWA WATU WATAKAOKUWA HAWAMCHI MUNGU BAADA YA HAYA.

Katika maandiko matakatifu, Mungu aliiadhibu miji ya Sodoma na Gomora na ile ya kando kando kutokana na uovu uliokuwa ukifanywa na watu wa miji hiyo. Tunasoma kuwa, Mungu aliiadhibu na kuipundua miji hiyo na kuifanya kuwa majivu kabisa. Lakini ni kwanini?

Biblia inatupa sababu nyingine ambayo tunaisoma katika waraka wa pili mtume petro kuwa, Mungu aliifanya hivyo miji hiyo ili pia IWE ISHARA AU MFANO KWA WATU AMBAO WATAKAOKUWA HAWAMCHI MUNGU BAADAE. 

[2 Petro 2:6] tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, AKAIFANYA IWE ISHARA KWA WATU WATAKAOKUWA HAWAMCHI MUNGU BAADA YA HAYA


Sasa nini maana ya ishara au ishara ni nini?

Ishara ni kitu kinachoashiria jambo fulani ambapo uwepo wake (yaani hiyo ishara), unawakilisha jambo fulani fulani.

Mfano: Ishara ya pundamilia barabarani inaashiria kivuko cha waenda kwa miguu, ishara ya pembe ya ndovu katika nembo ya Tanzania inaashiria utajiri wa wanyama pori nchini, ishara ya kuchanganya udongo inaashiria kumbukizi la TUKIO la muungano wa Tanganyika na Zanzibari, hivyo, mtu yo yote yule atakayeona ishara hizo, basi, zitampa taarifa moja kwa moja au zitamkumbusha kitu tukio fulani kwa urahisi na haraka zaidi kama vile ishara ya kuchanganya udongo linavyotukumbusha tukio la Muungano.


Vivyo hivyo pia katika miji ya Sodoma, Gomora na ile ya kando kando, Mungu pia aliifanya iwe ishara ya baadae kwa watu watakaokuwa hawamwogopi Mungu ili kusudi pale tutakapoona matendo yaliyopelekea miji ile kuangamizwa yakitendeka katikati yetu, basi, tukumbuke kile ambacho Mungu alichokifanya katika miji ile, hivyo tuogope kwa tutubu na kuyaacha mambo yetu maovu.


Ndugu mpendwa, unapoona mambo yaliyokuwa yakifanywa na watu wa sodoma na Gomora yanatenda katikati yako na tena kwa kasi kubwa, basi tambua kuwa Mungu anakuonya juu ya ghadhabu yake, hivyo ni wakati wa wewe kuacha dhambi zako na kumgeukia Mungu (usipoteze muda)


Unapoona na kusikia mamlaka za mataifa mbali mbali zikiharalisha na kupitisha kisheria mambo yaliyokuwa yakifanyika Sodoma na Gomora (ushoga), basi tambua ni muda wa kumtii Mungu kwa sababu ametoa ishara hiyo kwetu sisi watu wa baadae


[2 Petro 2:6] tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, AKAIFANYA IWE ISHARA KWA WATU WATAKAOKUWA HAWAMCHI MUNGU BAADA YA HAYA


Ni wakati wa kumgeukia Mungu kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na wala usiipuuzie hiyo ishara kwani Bwana alisema.

Luka 17:28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa KATIKA SIKU ZA LUTU, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; 

29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. 

30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. 

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.



MADA ZINGINEZO:


MADHARA YA KULISIKIA NENO LA MUNGU NA KUTOWAZA  KUCHUKUA UAMUZI WO WOTE ULE WA KULIFANYIA KAZI (KULITII)


Msaidizi wa kufanana naye ni nani ambaye Mungu alimfanyia Adamu? (Mwanzo 2:18)


USIMWACHE ALIYE CHEMCHEMI YA MAJI YA UZIMA.


Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema “Kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia” Je! Alikuwa akijigamba?(Wafilipi 3:6)



TABIA NYINGINE YA IBILISI UNAYOPASWA KUIFAHAMU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *