Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema “Kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia” Je! Alikuwa akijigamba?(Wafilipi 3:6)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Naomba kuuliza, hivi mtume Paulo alikuwa na maana gani au alilenga nini hasa kwa kusema “kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia? Je! Alisema hivyo kwa lengo la kujionesha na kujigamba?

Wafilipi 3:6 kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, KWA HABARI YA HAKI IPATIKANAYO KWA SHERIA SIKUWA NA HATIA

JIBU: Jibu ni hapana, Mtume Paulo aliposema hivyo, hakuwa na maana hiyo ya kujionesha wala kujigamba, la hasha! Kwa sababu kile alichokisema kilikuwa ni ukweli mtupu kwamba, kama kushika maagizo ya Mungu kwa kuutumainia mwili na kuifuata sheria, basi yeye hakuwa na hatia mbele za Mungu, na tena si yeye tu, walikuwepo na wengine wengi kama hao, mfano wazazi wake nabii Yohana mbatizaji (Zakaria na Elisabeti)

Luka 1:5 Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake ZAKARIA, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake ELISABETI

6 Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, WAKIENDELEA KATIKA AMRI ZOTE ZA BWANA NA MAAGIZO YAKE BILA LAWAMA

Lakini mtume Paulo aliposema hivyo alimaanisha nini hasa?


Jibu ni kwamba, mtume Paulo alisema hivyo kwa lengo la kuonyesha kuwa, hao watu wa madhehebu (Mafarisayo na Masadukayo), wanaojitumainisha katika sheria (torati), ambayo hawana hata ufunuo nayo wala uelewa wa yale yaliyoandikwa ndani yake kama alivyosema katika.

Warumi 2:17 Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu, 

18 na kuyajua mapenzi yake, na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati, 

19 NA KUJUA HAKIKA YA KUWA WEWE MWENYEWE U KIONGOZI WA VIPOFUMWANGA WAO WALIO GIZANI

20 MKUFUNZI WA WAJINGAMWALIMU WA WATOTO WACHANGA, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati; 

Kwamba, torati inanena habari za Yesu Kristo ambaye katika Yeye tunapata wokovu mkuu na wa thamani sana na si vinginevyo, na wala sio katika tamaduni za udhehebu (ufarisayo na usadukayo), kwa sababu yeye Paulo katika tamaduni hizo za sheria na udhehebu (ufarisayo), alikuwa ni zaidi ya wao, katika kushika sheria, na Juhudi, na TENA HAKUWA NA HATIA. Ndipo sasa alipoandika kwa kusema.

Wafilipi 3:4 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. MTU YE YOTE AKIJIONA KUWA ANAYO SABABU YA KUUTUMAINIA MWILIMIMI NI ZAIDI

NALITAHIRIWA SIKU YA NANENI MTU WA TAIFA LA ISRAELIWA KABILA YA BENJAMINIMWEBRANIA WA WAEBRANIAKWA HABARI YA KUISHIKA TORATINI FARISAYO

KWA HABARI YA JUHUDIMWENYE KULIUDHI KANISAKWA HABARI YA HAKI IPATIKANAYO KWA SHERIA SIKUWA NA HATIA


Hii inafunua nini?

Hata sasa wapo watu wengi kwenye dini zao na madhehebu yao, ambao kwa kweli na kwa dhati ni wenye juhudi kwa ajili ya Mungu kwa kushika sheria za dini zao na  madhehebu yao, na tena, Inawezekana ni wenye juhudi kushinda hata viongozi wao, sala za asubuhi mchana na jioni wapo, kwenye masifu ya asubuhi mchana na jioni wapo, kwenye Ibada za jumuiya wapo, kwenye misa za kutembeza masanamu nyumba kwa nyumba wapo, kwenye kukesha na kuwaomba malaika na wafu wawaombee kwa Mungu (machukizo kwa Bwana), wapo, kwenye michango na kujitoa kwa kila namna sawasawa na madhehebu yao wanashiriki kikamilifu kabisa, kwenye kutimiza maagizo ya kununua mafuta ya upako na maji ya upako wapo, kwenye kutimiza maagizo kupeleka kucha na nywele zao wapo, wanapodanganywa kubatiza watoto wachanga wapo, ni waaminifu na HAWANA HATIA katika sheria zote za dini zao na madhehebu yao (kama alivyokuwa Paulo katika udhehebu wake).


Lakini ndugu mpendwa, nataka nikwambie kuwa, hizo ni juhudi kwa ajili ya Mungu lakini si katika maarifa (Warumi 10:2). Pasipo Yesu Kristo na kuitii injili Yake iliyohubiriwa na mitume na manabii Wake watakatifu (sio dini yako wala dhehebu lako), ni kazi bure. 


Hivyo itii sasa injili ya Yesu Kristo na udumu katika mafundisho ya mitume kwa kutubu dhambi zako zote na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa kuzamishwa mwili wako wote katika maji na kwa jina la Yesu Kristo, nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu 

Matendo 2: 38 Petro akawaambia, Tubuni MKABATIZWE KILA MMOJA WENU KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)


LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, AU ATAKAYENENA KATIKA JINA LA MIUNGU MINGINE, NABII YULE ATAKUFA.


FUNZO KUTOKA KATIKA KISA CHA NADABU NA ABIHU.


BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO 


KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA KWANZA).

LEAVE A COMMENT