KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA KWANZA).

FUNDISHO MAALUMU KWA WALIOMWAMINI NA KUMPOKEA YESU KRISTO.

Shalom, jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, hili ni fundisho maalumu la kazi nyingine ya maandiko matakatifu kwa watu wote waliomwamini Yesu Kristo na kumpokea katika maisha yao (wafuasi wa Yesu Kristo). 


Lakini kabla ya kwenda mbele zaidi, inabidi tujue kwanza mfuasi wa Yesu Kristo ni nani kulingana na maandiko matakatifu (na sio kulingana na dini yako, dhehebu lako, utamaduni wa mababu zako wala wazazi wako).

Kulingana na maandiko, wafuasi wote na wote walio mwamini Yesu Kristo walibatizwa kwa jina lake (sio kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, bali kwa jina la Yesu Kristo). Tunalithibitisha hilo katika.

Matendo Ya Mitume 10:47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? 

48 Akaamuru wabatizwe KWA JINA LAKE YESU KRISTO. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. 

Soma tena

Matendo Ya Mitume 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Soma tena

1 Wakorinto 1:13 JE! KRISTO amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? AU JE! MLIBATIZWA KWA JINA LA PAULO

14 Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo; 

15 mtu asije akasema kwamba MLIBATIZWA KWA JINA LANGU

Na tena, kwa kuzamishwa mwili wote katika maji, kama ishara na kufa na kufufuka katika upya

Wakolosai 2:12 MKAZIKWA PAMOJA NAYE KATIKA UBATIZO; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. 

Soma tena.

Warumi 6:4 Basi TULIZIKWA PAMOJA NAYE KWA NJIA YA UBATIZO katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 

Na kupokea Roho Mtakatifu

Ni kama vile tu Waisraeli ambao walikuwa ni kanisa la kule jangwani (Matendo 7:38), walivyobatizwa wote katika wingu na bahari ili wawe wa Musa.

1 Wakorinto 10:2 WOTE WAKABATIZWA WAWE WA MUSA katika wingu na katika bahari; 

Ndivyo na sisi pia tunavyobatizwa kwa jina la Yesu Kristo kwa kuzamishwa katika maji ili tuwe wa Yesu Kristo.

Na kama vile kanisa la kule jangwani (Waisraeli), walivyounywea mwamba wa Roho, 

1 Wakorinto 10:4 WOTE WAKANYWA KINYWAJI KILE CHA ROHO; kwa maana WALIUNYWEA MWAMBA WA ROHO uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 

Na Ndivyo na sisi wote pia tuliomwamini Yesu Kristo tulivyonyweshwa kinywaji hicho (Roho Mtakatifu).

1 Wakorinto 12:13 Kwa maana KATIKA ROHO MMOJA  sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; NASI SOTE TULINYWESHWA ROHO MMOJA

Na ndio maana Bwana alisema.

Yohana 3:5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa KWA MAJI NA KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 

Hivyo kama ulibatizwa vinginevyo tofauti na maandiko, kwa kunyunyuziwa maji ya kwenye bakuri, au kuloweshwa kwenye paji lako la uso ulipokuwa mtoto mchanga, au kama ulibatizwa kwa jina lingine lo lote lile tofauti na La YESU KRISTO, basi tambua kuwa bado hujawa mfuasi wa Yesu Kristo, bali unajifurahisha katika uongo, hivyo unapaswa kurekebisha ubatizo wako na kuwa mfuasi wa Yesu Kristo kulingana na maandiko.

Kumbuka: Ni kulingana na maandiko matakatifu na sio dini yako wala dhehebu lako.

Usikose sehemu inayofuata…!!

Bwana akubariki, Shalom.


MADA ZINGINEZO:

UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?


NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.


Je! Ni dhambi kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali?


Waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 

NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI.

2 thoughts on - KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA KWANZA).

LEAVE A COMMENT