JE! NI KWELI MARIAMU MKE WA YUSUFU NI MALKIA WA MALAIKA, MANABII, MITUME, NA WATAKATIFU WOTE?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Naomba kuuliza, hivi ni kweli kuwa, Mariamu mke wa Yusufu ni Malkia wa malaika, manabii, mitume na watakatifu wote? Kwa sababu ndivyo ilivyoandikwa katika LITANIA ya Mariamu.

Malkia wa Malaika …………..        

utuombee

Malkia wa Mababu …………..

 utuombee

Malkia wa Manabii ………….. 

utuombee

Malkia wa Mitume ………….. 

utuombee

Malkia wa Mashahidi ………….. 

utuombee

Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee

Malkia wa Mabikira ………….. 

utuombee

Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee

Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee

Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee

Malkia wa amani ………….. 

utuombee


JIBU: Hakuna sehemu yo yote ile kwenye maandiko matakatifu palipoandikwa Mariamu mke wa Yusufu ni Malkia wa chochote kile, (hicho kitu hakipo popote pale kwenye maandiko), na wala maandiko hayajasema kuwa malaika, Manabii, mitume, na watakatifu wote wanaye malkia, huo ni uongo na mafundisho ya uongo kutoka kwa baba wa uongo (ibilisi), yaliyokinyume na maandiko matakatifu, kwa sababu mitume  na manabii watakatifu wa Bwana hawajawahi kuhubiri kitu kama hicho popote pale, na kama wewe unayesoma ujumbe huu unaamini hivyo au ulikuwa ukiamini hivyo siku zote za maisha yako, basi tambua kuwa ulidanganywa, na ukitaka kuthibitisha hilo, chukua biblia yako mfuate kiongozi wako na umuulize ni wapi ilipoandikwa Mariamu ni Malkia wa malaika, manabii, mababu, watakatifu au malkia wa chochote kile. Akishindwa mwache (huyo ni kiongozi kipofu wa vipofu).


Hata Katika ufahamu wa kawaida tu (pasipo ufunuo wo wote ule wa Roho), Malaika wanawezaje kuwa na nguvu na uwezo kuliko mkubwa wao Malkia? (ambaye injili ya uongo inamtaja kuwa ni Mariamu), kwa sababu maandiko yanasema Malaika wana nguvu na uwezo kuliko wanadamu. (Na Mariamu alikuwa ni mwanadamu).

2 Petro 2:11 Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa MALAIKA AMBAO NI WAKUU ZAIDI KWA UWEZO NA NGUVU, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana. 

Au Malkia wa Malaika anawezaje kuogopa na kuhofu mbele ya malaika wake hadi malaika wake anamwambie usiogope?

Luka 1:30 MALAIKA AKAMWAMBIAUSIOGOPEMARIAMU, kwa maana umepata neema kwa Mungu. 

Malaika hawana malkia yo yote yule, Maandiko yanasema wanaye Mfalme Mmoja tu, Bwana wa majeshi.

Isaya 6:2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

4 Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.

5 Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona MFALME, BWANA WA MAJESHI. 

Na pia manabii, mitume, na watakatifu wote, maandiko hayajasema kama wanaye malkia yo yote yule, bali Mfalme, ambaye wanamtazamia siku ile kama maandiko yanavyosema.

Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; 

21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake. 

Soma tena 

1 Timotheo 6:14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 

15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 

Na mababu pia kama wakina Ayubu, nao wanamtazamia Bwana, Mfalme na Mwokozi huyo huyo, atakayeibadilisha miili ya udhaifu na kutupa ile ya Utukufu.

Ayubu 19:25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.

26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; 

Hivyo fundisho hilo la kusema Mariamu ni Malkia wa malaika, mitume, manabii na watakatifu wote ni la uongo, na wewe unayesema maneno hayo katika LITANIA hiyo unasema uongo, na waongo wote hawana sehemu katika ufalme wa Mungu.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Mariamu Magdalene alikuwa ni mtume? (Yohana 20:17) 


Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.


ONYO..!! EPUKA KUTOA MANENO YA UONGO KATIKA SALA ZAKO.

LEAVE A COMMENT