ONYO..!! EPUKA KUTOA MANENO YA UONGO KATIKA SALA ZAKO.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Biblia inasema katika..

Matayo 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, NA KWA MANENO YAKO UTAHUKUMIWA. 

Kumekuwa na baadhi ya watu ambao kwa kukosa maarifa, wanajikuta wanatoa maneno ambayo ni kinyume na maandiko matakatifu katika sala zao, hii ni kutokana na kuwa wavivu kuchunguza na kusoma Biblia zao, au kudanganywa na dini za uongo na mitume wa uongo ambao wanajigeuza na kuwa mfano wa mitume wa Kristo..

2 Wakorinto 11:13 Maana watu kama hao ni MITUME WA UONGO, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 

Na tena inasema katika..

2 Timotheo 3:5 WENYE MFANO WA UTAUWA, LAKINI WAKIKANA NGUVU ZAKE; hao nao ujiepushe nao. 

Maneno hayo ya uongo yanapatikana katika salamu Maria ambayo inasema..

Salamu Maria
Umejaa neema
Bwana yu nawe
UMEBARILIWA KULIKO WANAWAKE WOTE
Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa
Maria Mtakatifu
Mama wa Mungu
UTUOMBEE SISI WAKOSEFU
Sasa, na saa ya kufa kwetu.

Amina.


Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza sema ni sala safi mbele za Mungu, na tena inayo mameno kutoka katika maandiko matakatifu ambayo Elisabeti mama yake Yohana Mbatizaji aliyasema, lakini si kweli, sala hii inayo maneno ya uongo ambayo ibilisi ameyapindisha kutoka kwenye maandiko kama tu anavyopindisha maandiko mengine kwa sababu Elisabeti hakuwahi kamwe kusema kuwa, Maria AMEBARIKIWA KULIKO WANAWAKE WOTE, bali alisema amebarikiwa KATIKATI WANAWAKE. Tunalithibitisha hilo katika..

Luka 1:42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. 

Hii ikiwa na maana kwamba, wapo wanawake wengine wengi waliobarikiwa na Mariamu akiwa miongoni mwao, sasa maneno ya uongo unayoyasema katika sala yako kuwa, amebarikiwa kuliko wanawake wote yametoka wapi wakati biblia haijasema hivyo? Muulize huyo kiongozi wako, tena akikuuliza mwanamke gani mwingine aliyebarikiwa katika biblia mwambie Hana, Sara, mke wa Manoa, bibi yake na mama yake Timotheo, na Yaeli, ambaye biblia inasema maneno haya juu yake..

Waamuzi 5:24  Atabarikiwa Yaeli KULIKO WANAWAKE WOTE; Mkewe Heberi, Mkeni, Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani. 

Akishindwa kukupa jibu lisiloeleweka, basi, ACHA MARA MOJA KUSEMA UONGO HUO KWENYE HIYO SALA YAKO, kwani utahukumiwa kwa hilo neno usiloweza lithibitisha katika biblia yako.

Na tena muulize ni wapi biblia iliposema kuwa, Maria anatuombea sisi wakosefu au Maria ni kipatanishi cha wenye dhambi na Mungu? Wakati biblia haisemi hivyo na badala yake inasema..

1 Timotheo 2:5  Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 

Akikwambia Bwana Yesu aliombwa na mama yake kwenye harusi ya kana walipotindikiwa na divai, mfungulie hapa asome>>>>Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokwama? (kulingana na Yohana 2:3-5)

Akikupa jibu lisoloelewaka, basi acha kusema huo uongo mbele za Mungu katika sala yako kuwa, Maria anakuombea wewe mkosefu sasa na saa ya kufa kwako, kwani kwa neno lako hilo ambalo huwezi lithibitisha kwenye maandiko utahukumiwa, na tena ondoka huko, usikubari kufungiwa ufalme wa mbinguni na viongozi vipofu na wanafki, wasiotaka kukufundisha ukweli wa kwenye maandiko matakatifu bali ukweli wa mashirika yao, wanaoshindwa kuwa waaminifu katika neno la Mungu bali katika mashirika yao, kwani wao wenyewe hawaingii..

Matayo 23:13  Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! KWA KUWA MNAWAFUNGIA WATU UFALME WA MBINGUNI; NINYI WENYEWE HAMWIMGII, wala wanaoingia hamwaachi waingie. 

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokwama? (kulingana na Yohana 2:3-5)


Je! Ni kweli Mariamu mama yake Bwana Yesu alipalizwa mbinguni?


Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?


JINSI AMRI YA UPENDO INAVYOWAFANYA WATU WADUMU KATIKA DHAMBI


IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.

LEAVE A COMMENT