MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)

Siku za Mwisho, Uncategorized No Comments

Tofauti na watu wengi wanavyodhani kuwa, ukishatubu dhambi zako na kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu ndio basi, mambo yote yanakuwa yamekwisha, unachosubiria ni mbingu mpya na nchi mpya, lakini nataka nikwambie kuwa hicho kitu si sawa hata kidogo, kwani biblia haitufundishi hivyo, biblia inatufundisha kuwa, hatupaswi kulala kwani ibilisi ameshatangaza vita ili atuangushe (Ufunuo 13:17), na tena inasema…

1 Petro 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, KAMA SIMBA ANGURUMAYE, HUZUNGUKA-ZUNGUKA, AKITAFUTA MTU AMMEZE.

Ikiwa na maana, endapo tusiposimama thabiti katika kuomba na katika neno la Mungu, basi hapo tutamezwa tu, yaani kupotezwa na kuchukuliwa na makanisa ya uongo na mafundisho ya uongo yanayohubiriwa leo hii ambayo katika makala hii fupi tuona baadhi, na hii ni sehemu ya kwanza (01), karibu.


MAKANISA YANAYOCHUNGWA NA MAASKOFU NA WACHUNGAJI WANAWAKE


Biblia inasema hivi katika Isaya 3:12 

Isaya 3:12  KATIKA HABARI ZA WATU WANGU, watoto ndio wanaowaonea, NA WANAWAKE NDIO WANAOWATAWALAENYI WATU WANGU, WAKUONGOZAO WAKUKOSESHA, waiharibu njia ya mapito yako. 

Hapo inaposema “WATU WANGU” haina maana kuwa ni kila mtu aliyeumbwa na Mungu, hapana! Ila ni watu wale waliojitenga na udunia, waliotubu dhambi zao na kumwamini Kristo na kubatizwa kwa jina lake, hao ndio watu wa Mungu wanaozungumziwa hapo…

2 Wakorinto 6:16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, NAO WATAKUWA WATU WANGU

Hao ndio watu ambao Mungu analalamika juu yao, kuwa wanawake wanaowaongoza na kuwatawala (katika kanisa), ndio wanaowakosesha, ikiwa na maana kwamba, mwanamke hajepewa dhamana na Mungu ya kuchunga au kusimamia kanisa la Mungu.

Kanisa lolote lile linalochungwa na kusimamiwa na mwanamke sio kanisa la Mungu, hakuna sehemu yoyote ile katika biblia kulipoamriwa kanisa la Mungu kuchungwa na mwanamke, bali kinyume chake inakemea kabisa.

1 Timotheo 2:8 Basi, NATAKA WANAUME WASALISHE KILA MAHALI, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. 

Na tena inasema

1 Timotheo 2:12 Simpi mwanamke RUHUSA YA KUFUNDISHA, WALA KUMTAWALA MWANAMUME, bali awe katika utulivu.

13 KWA MAANA ADAMU NDIYE ALIYEUMBWA KWANZA, na Hawa baadaye. 

Na tena mtume Paulo anamsisitiza Timotheo kwa kumwambia..

1 Timotheo 3:14  Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu.

15 Lakini nikikawia, UPATE KUJUA JINSI IWAPASAVYO WATU KUENENDA KATIKA NYUMBA YA MUNGU, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 

Ikifunua kuwa, ikiwa watu hawaendi sawa sawa na maneno hayo (kwa kuwaruhusu wanawake kuwa maaskofu na wachungaji), basi hiyo sio nyumba Ya Mungu aliye hai, haijarishi kuna nini hapo, kwa sababu Kama ingekuwa ni nyumba ya Mungu aliye hai ni wazi watu wangeenenda kama inavyopaswa kuenenda katika nyumba ya Mungu.

Hivyo ndugu mkristo, ukijiona upo katika kanisa la namna hiyo jua kabisa huyo mwanamke anayekuongoza anakukosesha na maandiko matakatifu ya Mungu, unachotakiwa kufanya ni kumweleza ukweli, kama hataki toka hapo, hiyo ni roho ya Yezebeli.

Ufunuo 2:20  Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. 

Usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo, hizi ni siku za mwisho.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


MMEKWISHA KUSHIBA, MMEKWISHA KUPATA UTAJIRI, MMEMILIKI PASIPO SISI.


UMESHAIFAHAMU NA KUIPOKEA BARAKA YA IBRAHIMU KATIKA MAISHA YAKO .


USITUMAINIE HEKALU LA BWANA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *