MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)

Siku za Mwisho, Uncategorized 4 Comments


Jina la Mwokozi Wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele, karibu katika sehemu ya pili ya makala hii fupi inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayowapoteza watu wengi duniani nyakati hizi za mwisho, tumeshatazama moja huko nyuma katika sehemu ya kwanza, ikiwa ulipitwa na sehemu hiyo na unahitaji uchambuzi huo, basi unaweza tuandikia ujumbe kwa namba +255755251999 au +255625574252  

Hii ni sehemu ya pili (02) ya makala yetu, karibu.



MASHAHIDI WA YEHOVA.

Hii ni moja ya taasisi inayowapotosha na kuwapoteza watu wengi sana duniani kwa mafundisho yao potofu na ya uongo na injili nyingine kabisa ambayo inatoka moja kwa moja kwa shetani baba wa uongo.


Biblia inasema katika..

2 Petro 2:1  Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, KAMA VILE KWENU KUTAKAVYOKUWAKO WAALIMU WA UONGO, watakaoingiza KWA WEREVU UZUSHI WA KUPOTEZA, WAKIMKANA HATA BWANA ALIYEWANUNUA, WAKIJILETE UHARIBIFU USIOKAWIA.

NA WENGI WATAFUATA UFISADI WAO; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 

Watu hawa wanamkana Bwana moja kwa moja kwa mafundisho yao potofu ya baba yao ibilisi ambayo yapo kinyume na maandiko matakatifu. Ndugu, ikiwa upo chini ya taasisi hiyo na kukubaliana na mafundisho yao, nakuhakikishia kuwa, umefarakanishwa na injili ya kweli ya Kristo na kupofushwa na adui (endapo usipotaka kutubu dhambi zako na kubatizwa katika jina la Yesu Kristo na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu aliye muhuri wa Mungu na kudumu katika fundisho la mitume).

Watu hawa wanamkana Bwana wazizi kama mtume Petro alivyoandika kwa uweza wa Roho kwa mafundisho yao yanayosema kuwa, mtu hapaswi kumwamini Yesu Kristo tu peke yake ili apate wokovu, kinyume kabisa na neno linalosema..

Matendo Ya Mitume 4:12 WALA HAKUNA WOKOVU KATIKA MWINGINE AWAYE YOTE, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. 

Wanasema, mtu akiisha mwamini Yesu Kristo hana budi kumwamini na Baba yake (Yehova), wakati Yehova Mwenye alishatuhitumishia kwa kutuambia..

Marko 9:7  Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, MSIKIENI YEYE. 

Tena wanaenda mbali na mafundisho potofu yanayowafanya watu wastarehe katika shambi zao kwa kuwafundisha kuwa, adhabu ya dhambi ni kifo tu! hakuna mateso kuzimu na wala hakuna ziwa la moto, Yohova ni Mwenye upendo na hawezi angamiza watu kwa moto! Wamesahau kuwa Yehova Huyo Huyo ni moto ulao na ana upande wa pili (Warumi 11:22), wamesahau kuwa, Yehova Huyo Huyo Mwenye upendo aliangamiza viumbe vyote Sodoma na Gomora na miji ya kando kando (isopokuwa watu watatu tu!) kwa kunyesha moto na kiberiti kutoka mbinguni (Mwanzo 19:24), Wamesahau kuwa, Yehova Huyo Huyo aliwaangamiza Walawi walioasi kwa kumezwa na ardhi wakiwa hai wao na wake zao (Hesabu 16:32-33).

Ndugu, achana na hayo mafundisho potofu, kuzimu ipo na moto wa milele upo, wala usidanganyike, ukifa katika dhambi leo hii bila Yesu Kristo utaishia Jehanam, Bwana aliweka wazi hilo katika…

Matayo 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze KUIUA NA ROHO; afadhali mwogopeni yule awezaye KUANGAMIZA MWILI NA ROHO PIA KATIKA JEHANAM.

Kisha kufuatia ziwa la moto baada ya hukumu ya mwisho kama maandiko yanavyothibitisha hilo katika sehemu nyingi tu.

Warumi 2:7 wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; 

8 na wale wenye fitina, WASIOITII KWELI, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; 

DHIKI NA SHIDA JUU YA KILA NAFSI YA MWANADAMU ATENDAYE UOVU, MYAHUDI KWANZA NA MYUNANI PIA; 


Mpendwa, toka katika taasisi hiyo ya uongo na acha kushikamana na mafundisho yao potofu, acha kushikamana na watu wenye mafundisho potofu yanayo mkana Bwana kwa kusema Yeye ndiye malaika Mikaeli, acha kushikamana na watu wanaopinga karama za Roho Mtakatifu kama vile kunena kwa lugha, unabii, miujiza uponyaji n.k katika kanisa kwa kwa kisingizio kuwa zilikoma, wakati kanisa la Kristo linajengwa kwa hizo katika mwili mmoja (Warumi 12: 4-8). 


Watu wanaopinga karama za Roho Mtakatifu wanawezaje kuwa mashahidi wa Kweli wa Yehova wakati Yehova Mwenyewe alisema….

Matendo Ya Mitume 1:8 Lakini MTAPOKEA NGUVU, AKIISHA KUWAJILIA JUU YENU ROHO MTAKATIFU; NANYI MTAKUWA MASHAHIDI WANGU katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 

Kumaanisha kuwa, mashahidi wa Yehova wa kweli ni wale waliobatizwa na kupokea nguvu na kipawa cha Roho Mtakatifu ambazo ndizo hizo karama zake katika katika kanisa, sasa wewe shahidi wa yehova unayepinga karama za Roho Mtakatifu ni shahidi wa yehova gani wakati unapinga karama zake? hivyo basi, tambua kwamba, wewe ni shahidi wa yehova mwengine bandia (ibilisi), na huna budi kutii angizo walilopewa mashahidi wa Yehova Halisi (mitume na manabii), ili uwe miongoni mwa mashahidi wa YEHOVA WA KWELI

Matendo 2:38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 


Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;


Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Ni kweli mshahara wa dhambi ni mauti na si moto wa milele?


Mailaika mikaeli ndiye Bwana Yesu?


MWANAMKE ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE, JE!  NI UZAZI UPI HUO UNAOZUNGUMZIWA?


UMEFUNGULIWA KAMA BARABA?


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)

4 thoughts on - MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)
  1. MUNGU awabariki sana waandaaji wote wa hii makala..,,nafahamu hii ni kweli itakayowakwaza wengi sana, hasa wafuasi wa makanita husika..,lakini KWELI ni lazima ihubiriwe..,ili tunusuru nafsi zetu..,na Nafsi za vizazi vijavyo..,,Natamani kuendelea kujifunza zaidi..,,
    Shalom..,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *