Mailaika mikaeli ndiye Bwana Yesu?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

JIBU: Hapana, malaika Mikaeli siye Bwana Yesu. Kumekuwa na mafundisho potofu yaliyoingizwa kwa welevu na shetani kupitia waalimu wa uongo na hata kusomba baadhi ya watu kuwa, malaika Mikaeli ndiye Bwana Yesu. Hayo ni mafundisho yaliyoingizwa kwa welevu na hata kumkana Bwana mwenyewe, ndugu toka huko.

2 Petro 2:1  Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. 

2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa

Mikaeli ni malaika ambaye yupo mahususi kwaajiri ya vita, kwaajiri ya kutetea ufalme wa Mungu. Na yeye ndiye mkuu wa malaika wote wa vita au kwa lugha rahisi ni jemedari wa vita.

Ufunuo 12:7  Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 

Maandiko yanasema kuwa, Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka. Sentensi hii inaonesha kuwa kuna kundi maalumu la malaika ambao kazi yao ni vita tu, kazi yao ni kupigana tu, kwasababu kuna malaika Wengine kazi yao ni sifa, wanasifu na kuabudu mbele ya kiti cha enzi milele na milele usiku na mchana (ufunuo4:8), sasa ni wazi kuwa malaika hawa wa sifa hawakuhusika kwenye hii vita.

Mikaeli siye Yesu Kristo, kwani hata malaika huyu mkuu mikaeli alionesha hali ya utii kwa Bwana wake, alionesha kuwa yeye hana uwezo zaidi ya Bwana wake.

Yuda 1:9  Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee. 

Bwana aliyezungumziwa hapo ni Yesu Kristo kwani yeye yupo juu ya vitu vyote, vya Mbinguni na duniani na yeye ndiye Mungu, hivyo ni wazi kuwa mikaeli siye Yesu.

Warumi 9:5  ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina. 

Bwana Yesu ndiye Anayewamiliki malaika wote, na malaika wote wanapanda na kushuka mbele zake akiwemo Na mikaeli 

Yohana 1:51  Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu. 

Anaposema malaika wa Mungu anamaanisha ni malaika wake, kwani Bwana Yesu ndiye Mungu mwenyewe katika mwili na ndio maana sehemu nyingine anasema kuwa atawatuma malaika zake.

BWANA YESU ni Mungu na wala sio mikaeli na ndio maana wayahudi walimshuhudia kuwa anakufuru kwa kujifanya yeye ni Mungu, kuonesha kuwa Bwana Yesu alikua akithibitisha kwa siri kuwa yeye ni Mungu na wayahudi waliona kuwa huyu anakufuru, hakuwa anakufuru bali ni kweli yeye ni Mungu (kama Tomaso alivyothibitisha)

Yohana 10:33  Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. 

Kuna maandiko baadhi, wengi wanayatafsiri isivyopaswa mafano andiko hili 

1 Wathesalonike 4:16  Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 

Wengi husema kuwa Bwana Yesu atakuja na sauti ya malaika mkuu hivyo sauti ya malaika mkuu ipo ndani yake na kuhitimisha kuwa kama ndani yake kuna sauti ya malaika mkuu basi ndiye mikaeli. Sasa kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa mikaeli ni Mungu kwani atakuja na parapanda ya Mungu, hivyo kama parapanda ya Mungu ipo ndani yake basi yeye ni Mungu. Umeona hapo? Kitu ambacho sio sahihi mikaeli hawezi kuwa Mungu, ila maandiko yameelezea vizuri kuwa Bwana atatuma malaika zake pamoja na hiyo parapanda na hiyo sauti ya malaika mkuu.

Matayo 24: 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. 

Ndugu yangu mikaeli ni malaika na sio Bwana Yesu, Bwana Yesu ni Mungu mwenyewe katika mwili na hii ni siri (1Timotheo 3:16) 

Maandiko yanasema kuwa kila goti litapigwa mbele za Mungu na sehemu nyingine mbele ya kiti cha enzi cha mwana-kondoo. Sasa hapa haimaanishaa kuwa kutakuwa na viti viwili vya Enzi kwamba utaenda mbele za Mungu na kisha mbele za Bwana Yesu hapana bali kiti cha enzi ni kimoja cha Bwana wetu na Mungu wetu Yesu Kristo. Uamini, usiamini ila siku moja utakuja kubali kwamba Kristo ni Bwana.

Hivyo ndugu yangu achana na hayo mafundisho yanayokwambia kwamba Bwana Yesu ni mikaeli, hayo ni mafundisho potofu na injili nyingine isiyo ya Kristo 

Wagalatia 1:8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 

9  Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. 

Bwana akubariki.


Mada zinginezo:

Je! Ni dhambi kibiblia kuwaomba wafu (watakatifu)?


Je biblia inaruhusu kubatizwa kwa ajili ya wafu?(1Wakorintho 15:29)


UMESHAIFAHAMU NA KUIPOKEA BARAKA YA IBRAHIMU KATIKA MAISHA YAKO .


NI KWA NAMNA GANI BWANA YESU ALIKUJA KUTIMILIZA TORATI NA MANABII?

LEAVE A COMMENT