NI KWA NAMNA GANI BWANA YESU ALIKUJA KUTIMILIZA TORATI NA MANABII?

Shalom, Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo apewe sifa milele na milele, karibu tuyatafakari maandiko na leo tutatazama ni kwa namna gani Bwana Yesu alikuja kutimiliza torati na manabii

Matayo 5:17   Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 

18   Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Sasa utajiuliza, kwanini ni Bwana Yesu tu ndiye aje kuitimiliza torati? Kwanini asiwe mtu mwengine? Jibu ni kwamba Bwana Yesu ndiye aliyeandikiwa mambo yote kwenye torati na Manabii

Yohana 1:45  Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 

Hivyo basi, mambo yote ya kwenye torati na manabii yalikua yanamuhusu yeye na ndio maana Paulo alisema kuwa mambo hayo ni KIVULI cha mambo yajayo bali MWILI ni wa Kristo 

Wakolosai 2:16  Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; 

17  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. 

Hapo anaposema mwili na kivuli ni kwamba, mwili siku zote huwa una kuwa na kivuli, mfano: ukisimama juani utakiona kivuli chako, lakini kivuli chako si wewe bali mwili wako ndio wewe. Hivyo hivyo na kwa torati navyo, ilikua ni kivuli lakini mwili ni wa Bwana Yesu.

Kama tulivyoona kuwa, kila kitu kwenye torati na manabii kinamuhusu mkuu wa Uzima, sasa tutazame mifano baadhi na kisha tutaelewa. 

Mfano: Kwenye torati makuhani walipaswa kutoa sadaka na dhabihu za dhambi kila baada ya muda fulani kutegemeana na dhambi, lakini sadaka hizo zilikua ni kivuli tu ila zilimuhusu Bwana Yesu mwenyewe ambaye alitolewa sadaka mara moja tu pale msalabani.

Waebrania 10:6  Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; 

7  Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. 

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), 

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. 

10  Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. 

Hivyo basi, Bwana Yesu alikuja ili kutimiliza hizo sadaka hapo, kufunua kuwa zilikuwa zinamuhusu yeye.

Kwenye torati pia kuna siku kuu saba ambazo ziliamriwa zishikwe (ukitaka kufahamu siku kuu hizi saba tuachie ujumbe wako kwenye sanduku la maoni) Ambazo ni pasaka, mzaliwa wa kwanza n.k ambazo kimsingi zinamuhusu Bwana Yesu kwani yeye ndiye pasaka wetu na pia ndiye mzaliwa wa kwanza wa walio kufa

Wakolosai 1:18  Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 

Umeona? Hivyo ndivyo alivyokuja kuitimiliza torati na manabii, sehemu nyingine kwenye (Zaburi 22:18) Maandiko yanasema kuwa walipigia vazi langu kula na haya maneno yalimuhusu Bwama Yesu, hivyo ile siku wale askari walipolipigia kula vazi lake kukatimiliza hilo andiko. Kuna maamdiko mengi sana ambayo hatuwezi elezea yote hapa, ila ni jukumu lako kusoma na kumjua Mungu kwa viwango vingine.

Lakini nini tunachojifunza kweye hiyo mifano michache? Ni kuwa utimilizwaji wa torati na manabii bado haujakamilika kwani maneno mengine ya unabii aliyoandikiwa Bwana Yesu bado hayajatimia mfano.

Yuda 1:14  Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, 

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. 

Soma tena

Isaya 24:3  Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo. 

Ujio wa Bwana Yesu ulikuwa ni sehemu ya utimilizwaji wa torati na manabii na ndio maana hadi leo mbingu na nchi bado hazijapita, lakini Bwana atakapoyatimiza yote, hizi mbingu za sasa zitapita na Bwana atazifanya mpya ambazo tutaishi kwa raha na amani, pasipo dhambi wala mauti, Na pia Bwana alisema maneno haya katika 

Yohana 14:3  Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 

Je! Bwana akija dakika mbili mbeleni utaenda nae? Kama huna uhakika huo ni kwanini usimpokee leo kwenye maisha yako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni kwa wa maji mengi na kwa jina la Yesu? Ndugu yangu, amua kumpokea leo Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako.

Bwana akubariki. Shalom 


Mada zinginezo:

Mana ni nini katika maandiko?


Pazia la Hekalu ni nini katika biblia?


MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.



Ni Mtume gani aliyekuwa Mkuu na Wa kwanza  kuliko wote katika biblia?


Bado Bwana Yesu anasema nawe kwa mifano?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *