Jibu: Ndio ni dhambi kulingana na biblia kuwaomba wafu (watakatifu) na ni machukizo makubwa sana Mbele za Mungu.
Kuna watu wanaamini mapokeo yanayosema kuwa, tunaweza kuwaomba wafu ambao ni watakatifu walioishi maisha matakatifu hapa duniani kutuombea kwa Mungu, mafundisho ambayo si sahihi kwani hayatokani na Mungu bali wanadamu kama Bwana alivyosema katika
Marko 7:7 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,
8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
Hata ukichunguza katika maandiko, utagundua kulikuwapo na watu wengi sana ambao waliishi maisha ya kumpendeza Mungu na hadi Mungu mwenyewe aliwasifia. Mfano wa mtu huyu ni Ibrahimu na waisrael wote walifahamu historia ya maisha yake, lakini huwezi kuona mahali popote katika maandiko wana wa Israel wakimtaja Ibrahimu kuwa awaombee mbele za Mungu.
Lakini pia utaona hata kwa Nabii Musa ambaye alitembea na Mungu kwa ishara na miujiza mingi katikati ya wana wa Israel, hakuwahi kutajwa na wana wa Israel katika sala na dua zao kuwa awaombee kwa Mungu, wote waliomba kwa Mungu na tunaweza thibitisha hilo katika
2 Mambo ya Nyakati 32:20 Na kwa ajili ya hayo HEZEKIA MFALME, NA ISAYA NABII, MWANA WA AMOZI, WAKAOMBA, WAKALIA HATA MBINGUNI.
2 Wafalme 19:15 Naye Hezekia AKAOMBA MBELE ZA BWANA, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
2 Wafalme 6:17 Elisha AKAOMBA, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
Unaona? Kati ya hao, hakuna hata mmoja aliyemuomba Musa nabii au Ibrahimu au Yusufu awaombee kwa Bwana, wote waliomba kwa Bwana wala si kwa wafu (watakatifu) akina Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, watu ambao Bwana mwenyewe alithibitisha kuwa tutawaona katika ufalme Wake
Luka 13:28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, MTAKAPOMWONA IBRAHIMU NA ISAKA NA YAKOBO na MANABII WOTE KATIKA UFALME WA MUNGU, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Hata wana wa Israel kipindi wanatoka Misri kuelekea nchi ya ahadi, utagundua kuwa Waliomba kwa Bwana, Musa alienda kwa Bwana kuomba na wala hakumtaja Ibrahimu wala mtakatifu fulani aliyekufa kuwa awaombee kwa Bwana
Hesabu 11:2 Ndipo watu wakamlilia Musa; naye MUSA AKAMWOMBA BWANA, na ule moto ukakoma.
Unaona hapo? Hakuombwa Ibrahimu wala Musa wala Daudi wala Isaya wala Daniel wala Ezekiel Wala Yeremia, na biblia imeweka wazi kabisa kuwa yoyote awaombaye wafu anafanya MACHUKIZO mbele za Bwana soma
Kumbukumbu La Torati 18:10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE WAFU.
12 KWA MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
Na WACHUKIZAO wote sehemu yao ni katika ziwa la moto (ufunuo 21:8)
Usiseme hao ni watu wa agano la kale, ndugu yangu, safari ya wana wa Israel kutoka misri kwenda nchi ya ahadi inafananishwa na sisi wakristo tunaoelekea nchi yetu ya hadi mbinguni hivyo basi, kama wao hawakuwaomba wafu (watakatifu) akina Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu n.k basi na sisi hatupaswi kuwaomba wafu (watakatifu) kama akina Petro, Yohana, Paulo, Barnaba, Bikira Maria n.k kwani kwa kufanya hivyo tutakua tunafanya machukizo mbela za Mungu wetu, wote tunapaswa kumwomba Bwana kama hao nao walivyomwaomba.
Kama una hiyo tabia acha mara moja na kama kanisa linafundisha hivyo mweleze kiongozi wako na kama hataki kuelewa basi toka hapo mara majo ukatafute sehemu sahihi kwani haijarishi ni wangapi mnaamini hivyo Bwana ataangamiza wote kama ulimwengu ule wa Nuhu.
Shalom.