Shalom, karibu tuyatafakari ya maneno ya uzima. Leo tutaangalia mada inayosema kuwa, Mungu ana nafsi tatu?
Mandiko sehemu kadhaa yanathibitisha kuwa, Mungu ni mmoja tu, aliyevifanya vitu vyote, vya baharini na nchi kavu, vinavyoonelana na visivyoonekana. Lakini sasa baadhi ya wakristo wanaenda mabali na kudiliki kusema kuwa, Mungu ni mmoja ila ana nafsi tatu, sasa jambo hili ni sawa kulingana na maandiko? Jibu ni la! Mungu hana nafsi tatu kwani yeye mwenyewe alivyoapa alisema hivi
Mwanzo 22:16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
Soma tena
Yeremia 49:13 Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
Kwa maandiko hayo sasa, kama Mungu angekuwa na nafsi tatu ni wazi angesema kuwa KWA NAFSI ZANGU nimeapa au KWA NAFSI ZETU tumeapa.
Kwa kukosa ufunuo, viongozi wengi wanamshusha hadhi Bwana pasipo kufahamu kwa kusema kuwa kuna Mungu baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu, kitu ambacho si sahihi.
Ukisema kuwa Kristo ni nafsi, sasa mbona Kristo mwenyewe na yeye ana nafsi?
Wagalatia 1:4 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.
Sasa hapo ni nafsi tatu kweli? Kama Mungu ana nafsi tatu ambazo ni Mungu Baba, Mwana, na Roho mtakatifu mbona mwana mwenyewe na yeye anayo nafsi yake? Basi Mungu anazo nafsi zaidi ya tatu, unaona?. Hivyo basi, Mungu hana nafsi tatu bali ana nafsi moja kama alivyosema pia katika Isaya
Isaya 45:23 Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Sasa huyu Mungu mmoja ni nani?
Kwanza tufahamu kuwa Mungu ni Mungu mwenye wivu na wala utukufu wake hawezi mpa mwengine
Isaya 42:8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Soma tena
Isaya 48:11 Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.
Sasa Mungu huyu anafahamika na Ibrahimu, Isaka na Yakobo kama Mungu Mwenyezi. Lakini Kwa Musa na Daudi n.k anafahamika kama Yehova
Kutoka 6:3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Na kwa Paulo anafahamika kama Yesu Kristo
Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Sasa ukisoma maandiko utagundua kuwa Kristo alitabiliwa na ataitwa kwanza, mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele na Mfalme wa amani.
Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Sasa kama Kristo ni mwingine, Mungu angewezaje kumpa utukufu mkuu wa namna hii na yeye utukufu wake hampi mwingine? Ndipo utakapojua kuwa ni Mungu huyo huyo na ndio maana sehemu nyingine anafahamika pia kama Immanueli yaani Mungu pamoja nasi.
Na ndio huyu huyu aliyesema maneno haya katika
Matendo Ya Mitume 15:16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha; 17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
Kumbe jina la Mungu limetajwa na linatajwa katika matifa hadi leo hii, sasa ni jina gani hilo linalotajwa katika mataifa? Utagundua kuwa ni Yesu Kristo.
Na Roho mtakatifu sio nafsi ya Mungu, Roho mtakatifu ni Roho wa Mungu au Roho Bwana Yesu, na ndio maana sehemu nyingine maandiko yanasema ni Roho wa Bwana Yesu
Wafilipi 1:19 Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo;
Soma pia
Matendo Ya Mitume 16:7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,
Hivyo basi kama wanafunzi na mitume walimwagiwa Roho wa Bwana Yesu siku ya pentekoste, basi ni wazi kuwa Bwana Yesu ni Mungu na ndiye aliyetoa ahadi ya kumwaga Roho wake kama alivyomwambia nabii Yoeli na yeye ndiye aliyewamwagia Roho wake mitume na wanafunzi.
Hivyo basi Bwana Yesu ni Mungu mwenyewe katika mwili na si nafsi ya Mungu kama baadhi ya madhehebu yanavyodhani.
Bwana akubariki. Shalom
MADA ZINGINEZO:
Jina la BWANA (Mungu) ni Yesu Kristo?
FAHAMU NINI MAANA YA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24)
JE! KAMA BWANA YESU NDIYE MUNGU, KULE MLIMANI ALIENDA KUMUOMBA NANI? (Luka 6:12)
Je! Kuna Mungu wawili? (Kulingana na Yohana 1:1)
Bwana Yesu si Mungu mweza yote (Baba) kulingana na Yohana 14:28?