JE! KAMA BWANA YESU NDIYE MUNGU, KULE MLIMANI ALIENDA KUMUOMBA NANI? (Luka 6:12)

  Mungu, Uncategorized

SWALI: Biblia inasema kuwa, Yesu Kristo ndiye Mungu Mkuu (Tito 2:13), aliye juu ya mambo yote na mwenye kuhimidiwa milele na milele, Amina (Warumi 9:5). Na kumbuka hakuna Mungu wawili bali ni mmoja na ana nafsi moja tu kama maandiko yanavyosema katika (Amosi 6:8). Swali ni je! Kama Yesu Kristo ndiye Mungu, kule mlimani alienda kumuomba nani?

Luka 6:12 Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ILI KUOMBA, AKAKESHA USIKU KUCHA KATIKA KUMWOMBA MUNGU.

JIBU: Ni kweli kabisa kuwa, zipo sehemu kadhaa ambazo biblia imerekodi Kristo akiomba kwa Mungu na sio mlimani tu, lakini biblia hiyo hiyo pia inasema Yesu Kristo huyo huyo ndiye Mungu na Mwenye uweza peke yake, sasa hapo haina maana kwamba biblia inajichanganya la hasha! na wala sio kwamba Mungu amegawanyika katika sehemu tatu au nafsi tatu hapana! Kwani Mungu Mwenyewe alishasema hakuna mwengine yoyote aliye pamoja na Yeye.

Isaya 44:24 Bwana, MKOMBOZI WAKO, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; NI NANI ALIYE PAMOJA NAMI? 

Umeona?.. Lakini pia andiko hilo linasema kwamba, Mungu Muumba wa vitu vyote NDIYE MWOKOZI, sasa je! tuna Waokozi wawili? Kwa sababu Kristo nae ni Mwokozi, umeona hapo? Hivyo basi, tunamuhitaji sana Roho wa Yesu Kristo ili tuweze kumwelewa Bwana Wetu na Mungu Wetu Yesu Kristo na sio elimu zetu za theologia na falsa ambazo biblia imetuonya tujiadhari nazo.


Turudi kujibu swali letu.

Kwanza kabisa inatupasa tufahamu kuwa, maandiko matakatifu katika agano jipya yanasema kwamba, Mungu alidhihirishwa katika mwili (1 Timotheo 3:16). Swali ni kwanini? Kwa sababu hata katika agano la kale pia alijidhihirisha katika mwili na kula kunywa, hivyo ni lazima kuwe na sababu ya yeye kudhihirishwa katika mwili na moja wapo ya sababu ni kwamba, ili awe kielelezo kwetu sisi wanadamu katika safari yetu ya kukaa hapa duniani kwa sababu Yeye asili yake ni Roho (Yohana 4:24), hivyo ilimpasa ajidhihirishe katika mwili kwanza na kukaa pamoja nasi na kutupatia kielelezo (siri ya Uungu ni kubwa mno)

1 Timotheo 3:16 Na bila shaka sili ya utauwa ni Kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu. 

Soma tena

Isaya 35:4 Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.

5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

Ule mwili ambao Mungu alijidhihirisha ndani yake ndio ulioweza kukaa na wanadamu na kutoa maelekezo ya kufanya ikiwemo pamoja na kuomba, hivyo basi, MWILI ULIOMBA KWA ROHO (kutupatia sisi kielelezo) kwamba, na sisi kama Wakristo tunapaswa kufuata kielelezo kile kile cha ule mwili uliosuburiwa pale masalabani kwa Kuomba kwa Mungu tu ambaye ni Roho na ndiye Bwana huyo huyo (2 Wakorintho 3:17), Haleluya…!!!


Mtu yoyote yule anayejiita Mkristo harafu anaomba kwa Mariamu, anaomba kwa Yosefu, anaomba kwa matakatifu Athanasio, anaomba kwa Paulo, anaomba kwa malaika Mikaeli au Gabrieli, tofauti na kwa ROHO ambaye ndiye Bwana, anatenda dhambi na kufanya machukizo mbele za Mungu kwa sababu hafuati nyayo na kielelezo tulichoachiwa tayari juu ya jambo hilo la Kuomba.

1 Petro 2:21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, AKAWAACHIA KIELELEZO, MFUATE NYAYO ZAKE.

Mambo mengine tunayopaswa kufuata ni lazima kwenda kubatizwa kama ule mwili ulivyoenda kubatizwa, kupokea Roho Mtakatifu kama ule mwili nao, kujaribiwa kama ule mwili nao ulivyojaribiwa, kukesha na kuomba kama ule mwili nao, kudhihakiwa na kuchukiwa kama ule mwili nao, kutukanwa na kuambiwa tuna wazimu kama ule mwili nao, kuambiwa tuna mapepo kama ule mwili nao, kwani hatuwezi mzidi Yeye aliyetupa kielelezo maana imeandikwa

Matayo 10:25 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? 

Na tena, ule mwili ambao Mungu alidhihirishwa ndani yake ndio unaochukua Utukufu na sifa zote za kwenye biblia. Mchungaji Mkuu (1 Petro 5:4), Nabii Mkuu (Luka 7:16), Mtume Mkuu na kuhani Mkuu (Waebrania 3:1), Mungu Mkuu, mfalme kuu, Mwana wa Adamu, Adamu wa pili, Mwana wa Daudi, Masihi, Mwana wa Mungu, Musa wa pili, Mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana, jemedari wa vita n.k, sifa zote na Utukufu wote unamrudia Yeye Mwenyewe na hawezi mpa mwengine wala masanamu.

Isaya 42: 8 MIMI NI BWANA; NDILO JINA LANGU; NA UTUKUFU WANGU SITAMPA MWINGINE, wala sitawapa sanamu sifa zangu.

Je! Umeshatubu dhambi zako na kumwamini Yesu Kristo? Kama bado unangoja nini? Je! Ni nini kinachokuzuia usifanye hivyo? Basi mwamini leo Mkuu wa uzima na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa kuzamishwa katika maji tele na kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na (Matendo 2:38), ili upate ondoleo la dhambi zako.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

GEUKA KATIKA NJIA YAKO NA IRUDIE NJIA YA MUNGU.


MCHUNGAJI WAKO NI NANI?


BASI ‘BWANA’ NDIYE ROHO.


FAHAMU NINI MAANA YA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24)


Mungu ana nafsi tatu?

LEAVE A COMMENT