Je! Kuna Mungu wawili? (Kulingana na Yohana 1:1)

Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno ALIKUWAKO KWA MUNGU, NAYE NENO ALIKUWA MUNGU.

SWALI: Tukisoma kwenye Yohana 1:1 inasema kuwa, Neno alikuwa kwa Mungu, na Neno huyo na yeye pia alikuwa ni Mungu, sasa je! Kuna Mungu wawili kulingana na andiko hilo?

JIBU: Mungu ni mmoja tu! aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo na ndiye aliye juu ya vyote.

1 Wakorinto 8:6  lakini kwetu sisi MUNGU  NI MMOJA TU, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. 

Lakini ni nini hasa ambacho mtume Yohana alichokuwa akikimaanisha hapo? 

Ikumbukwe kwamba, wakati Bwana Yesu alipokuwapo duniani na wanafunzi wake, maandiko yanasema kuwa, sio kila kitu ambacho Bwana alichokifanya mbele yao au vitu vyote vilivyotokea mbele yao, basi, wanafunzi wake walivielewa vitu hivyo hapo kwa papo, hapana! vingine walikuja kuvielewa baadae kabisa, baada ya Bwana kufufuka, mfano; lile tukio la Bwana kupanda mwana punda na kuingia Yerusalemu, maandiko yanasema kuwa, hilo tukio wanafunzi wake hawakuelewa maana yake hadi baada ya Bwana kutukuzwa.

Yohana 12:14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, 

15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.

 16 MAMBO HAYO WANAFUNZI WAKE HAWAKUYAFAHAMU HAPO KWANZA; LAKINI YESU ALIPOTUKUZWA, NDIPO WALIPOKUMBUKA YA  KWAMBA AMEANDIKIWA HAYO, na ya kwamba walimtendea hayo. 

Lakini mbali na tukio hilo, hata lile tukio la Bwana kufufuka pale kaburini, Wanafunzi walioenda pale walikuwa bado pia hawajafahamu jambo hilo la kufufuka kwake  Bwana ijapokuwa Bwana alishawahi liongelea jambo hilo mbele yao.

Yohana 20:6 Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala, 

7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.

 8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini. 9 KWA MAANA HAWAJALIFAHAMU BADO ANDIKO, YA KWAMBA IMEMPASA KUFUFUKA. 

Umeona? Sio mambo yote waliyafahamu hapo hapo, mengine waliyafahamu baadae. Hivyo, hata jambo hilo la kwamba Neno, yaani Bwana Yesu kuwa ni Mungu, hawakuwahi kulifahamu kabla, ila walikuja kulifahamu baada ya muda. Lakini sasa, kabla ya kufahamu kuwa Bwana ni Mungu, kitu walichokuwa wakikifahamu  wanafunzi wale ni kuwa, Yesu Kristo alitoka kwa Mungu yaani alikuwa kwa Mungu (Mwana wa Mungu) 

Yohana 16:30  Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; KWA HIYO TWASADIKI YA KWAMBA ULITOKA KWA MUNGU. 

Hivyo, baada ya kufahamu hayo yote kwa pamoja kuwa, Kristo (Neno) ambaye pia ni  ni Nuru, alitoka kwa Mungu, na yeye Mwenyewe ndiye Mungu, ndipo sasa mtume Yohana alipoandika hivyo kuwa, Neno alikuwako kwa Mungu na yeye ndiye aliyekuwa Mungu huyo huyo, na wala hakumaamisha Mungu wawili pale.

Na jambo hilo hilo, Mtume Yohana aliliweka wazi pia katika waraka wake wa kwanza kuwa, nuru yaani Bwana Yesu, ndiye Mungu 

1 Yohana 1:5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, YA KWAMBA MUNGU NI NURU, wala giza lo lote hamna ndani yake. 

Soma tena

Warumi 9:4 ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; 

5 ambao mababu ni wao, NA KATIKA HAO ALITOKA KRISTO KWA JINSI YA MWILI. NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE, MUNGU, MWENYE KUHIMIDIWA MILELE. AMINA. 

Hivyo, kwa kuhitimisha ni kuwa, Mtume Yohana hakuzungumzia Mungu wawili pale,  ila ni mmoja tu! Yaani Yesu Kristo, na ambaye kila goti litapigwa mbele zake na kila ulimi utaapa mbele zake kama ilivyotabiriwa na nabii (Isaya 45:23)

ZINGATIA: Ukimwamini Bwana Yesu kuwa ni Mungu, au alitoka kwa Mungu, au Mwana wa Mungu, au ni Mwana-Kondoo wa Mungu, aliyekufa kwaajiri ya dhambi zako, kisha ukatubu na kubatizwa na kuishi maisha ya utakatifu kwa kuyafanya mapenzi yake, basi utaurithi uzima wa milele.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.


MADA ZINGINEZO:

Koga ni nini katika biblia?


Mede ni nini kama tunavyosoma katika Wafilipi 3:14?


Kufunua Marinda ni nini katika biblia? (Yeremia 13:26)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *