Mede ni nini kama tunavyosoma katika Wafilipi 3:14?

Wafilipi 3:14  nakaza mwendo, niifikilie MEDE ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. 

JIBU: Mede ni kitu cha thamani sana kinachotolewa kwa mtu fulani kama zawadi kutokana na kitu fulani alichokifanya kwenye ama mashindano au kutokana na kungundua kitu cha tofauti katika jamii, na mede hizi utolewa kulingana na kazi au kitu ambacho mtu alikifanya katika nafasi yake, kama ni katika nafasi ya kwanza, ya pili, n.k mede huwa ni kitu cha fahari sana kwa yule ko ambaye anakipokea, kwani, kina mfuta machozi au kumriwadha kutokana na kazi aliyoifanya katika mazingira ambayo hayakuwa rafiki kwa muda wote.

Vivyo hivyo na sisi pia tulio mpokea Bwana kwenye maisha yetu katika nafasi mbali mbali, huo ndio mwito wetu Mkuu katika Yesu Kristo kama alivyotujaalia yeye, hivyo tunawajibu wa kukaza mwendo kwa kufanya kazi ya Bwana wetu Yesu kristo, kwani kuna mede za thamani sana alizotuandalia za kutufuta machozi na kutufariji kwa kazi hizo, kama wewe ni mahubiri, basi, hubiri kwa nguvu zote, mwimbaji msifu Mungu kwa nguvu zote, mwalimu fundisha kwa nguvu zote, mwenye kusaidia kazi ya Mungu ya injili kwa mali zako fanya kwa nguvu zote, sote  tukitazamia mede hizi za thamani zilizopo mbele yetu. Hivyo kama ulipoa na kuzembea sehemu fulani katika kumtumikia Mungu, basi, hamsha nia yako tena sasa kwani yupo karibu sana kurudi na kutulipa sawasawa na kazi zetu huku tukidumu katika utakatifu.

Ufunuo 22:12  Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 

Bwana akubariki. Shalom 

Mada zinginezo:

NA HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO YONA.


Nini maana ya kuokoka katika biblia?


TAFUTA PESA!  TAFUTA PESA! 

3 thoughts on - Mede ni nini kama tunavyosoma katika Wafilipi 3:14?
  1. je! ina maana ili uwe mkristo nilazima uwe nahuduma kanisani? na je wale walio tu wakristo wasio nahuduma wajibu wao ni upi?

  2. je ili uwe mkristo nilazima uwe nahuduma fulani kanisani? au wale walio wakristo wasio nahuda wajibu wao ni upi?

  3. Ili uwe mfuasi wa Yesu Kristo ni lazima utubu dhambi zako na kubatizwa kwa jina lake na kupokea Roho Mtakatifu, Kisha katika udumu katika mafundisho ya mitume ambapo Mungu atakutumia sawasawa na mapenzi yake ya kukuita kwake katika neema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *