Nini maana ya kuokoka katika biblia?

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Swali hili limekua likiulizwa na watu wengi sana hasa pale unapowafuata kuwahubiria habari njema za wokovu na ujio wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, wengi watakuuliza ama kwa dhihaka tu au kwa lengo la kutaka kufahamu, au kwa kujiona wanafahamu zaidi lakini kimsingi hakuna wanachofahamu, zaidi ni maneo tu ambayo walisikia na kuambiwa na kuyakubari pasipo wao kutaka kuufahamu ukweli kwa kuchunguza, Bwana atusaidie sana. Sasa leo kwa neema za Bwana tutaenda kutazama nini maana ya kuokoka kibiblia na umuhimu wake.

Lakini kabla hatujaelezea maana ya kuokoka kimaandiko, hebu tuangalie neno hili katika lugha isiyo ya kibiblia.

Kuokoka ni kitendo cha kutoka  sehemu moja ambayo ni hatari na kwenda sehemu nyingine ambayo ni salama.

Mfano: mtu aliyepona na ajari ya moto katika nyumba, tunaweza sema kuwa, mtu huyo AMEOKOKA na ajari ya moto, yaani ametoka sehemu ambayo ni hatari (penye moto) na kwenda sehemu ambayo ni salama

Hivyo basi, kibiblia pia, neno kuokoka linahusisha vitu viwili ambavyo ni hatari iliyopo na upande wa salama. Kwa kuanza na hatari iliyopo tunasoma katika 

Isaya 28:22   Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; MAANA NIMESIKIA KWA  BWANA, BWANA WA MAJESHI, HABARI YA HUKUMU ITAKAYOTIMIZWA, NAYO IMEKUSUDIWA, ITAKAYOIPATA DUNIA YOTE PIA. 

Unaweza pitia kwa muda wako vifungu hivi Isaya 13:6-8. Isaya 13:9-13

Umeona? Kumbe kuna siku ya hatari sana inayokuja mbeleni ambayo Ipo tayari kutimizwa juu ya uso wa dunia na juu ya wanadamu wote watendao maovu, lakini Bwana kwa huruma zake ametuwekea sisi wanadamu njia ya ukombozi, njia ya kututoa kwenye hii hatari na kwenda sehemu ambayo ni salama ambayo ni kwake yeye MUNGU MWENYEZI  na njia hii si nyingine zaidi ya Bwana Yesu.

Na lengo la ghadhabu hii ni kuteketeza uovu, sasa endapo uovu utakuwa ndani ya mwanadamu basi huyo mwanadamu naye atateketezwa. Sasa wanadamu wanaotenda uovu ni wapi? Soma

Warumi 1:18   Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. 

Umeona? Kumbe mwanadamu yeyote anayeipinga kweli basi huyo anatenda uovu, haijarishi anafahamu au la! Mtu yeyote anayeipinga injili ya Bwana Yesu huyo tayari anatenda uovu na hii ghadhabu inamuhusu.

2 Wathesalonike 1:8  katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; 

Bwana Yesu alitoa nafasi kwa wanadamu wote kwa kusema maneno haya

Marko 16:15   Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 

16  Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 

Umeona hapo? Bwana alisema kuwa yeyote atakayeamini injili yake na kubatizwa katika ubatizo sahihi basi huyo ataokoka, ataokoka na nini? Ataokoka na hii ghadhabu juu wote waliosalia ambao hawajaitii injili ya Bwana.

Hivyo basi, maana ya kuokoka ni kuitii injili ya Bwana Yesu na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu na kupokea kipawa cha Roho mtakatifu na kuishi maisha matakatifu kwa kufanya mapenzi ya Mungu.

Ndugu yangu, ukiona umebatizwa kwa kunyunyuziwa vimaji basi fahamu kuwa hiyo si injili ya Bwana Yesu, hivyo tafuta ubatizo sahihi kwani utakua hujaitii injili ya Bwana na utaangamia, ukiona hadi leo unaomba wafu au watakatifu fulani, fahamu kuwa hujaitii injili ya Bwana Yesu wewe, hivyo tubu na uache hizo ibada la sivyo utaangamia, ukiona hukemewi uvaaji wa suruali na vimini Kanisani kwako, upakaji wa make up, mawigi, rasta, kucha za bandia, basi fahamu kuwa bado hujaitii injili ya Bwana Yesu hivyo acha mara moja kwani hii ghadhabu itakuhusu, ukiona Kanisani kwenu wanapinga maagizo ya Bwana kama kushiriki meza ya Bwana, kutawadhana miguu na Wanawake kufunika vichwa wakati wa ibada, basi jua hujaitii injili ya Bwana hivyo unaitaji uitii ili uokoke na hiyo ghadhabu.

Je! Umeshaokoka na hii ghadhabu kwa kuitii injili ya Bwana Yesu? Kama bado unasubiri nini? Fanya haraka maana mida tulionao ni mchache sana.

Marko 1:15  akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. 

Bwana akubariki. Shalom 


Mada zinginezo:

Je ubatizo sahihi ni kwa jina la Yesu au Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?


JINSI AMRI YA UPENDO INAVYOWAFANYA WATU WADUMU KATIKA DHAMBI


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.


Mbegu iharibikayo ni ipi? (1 Petro 1:23)


Kivipi Mungu ni Mungu wa miungu, je hao miungu ni masanamu?

5 thoughts on - Nini maana ya kuokoka katika biblia?

LEAVE A COMMENT