Je kubandika picha ya yesu au kuweka vinyago nyumbani ni dhambi?

Dhambi, Uncategorized No Comments

SWALI: Je kubandika picha au kuweka vinyago nyumbani ni dhambi?

Kwani biblia inasema..


Kutoka 20:4
[4]Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.


JIBU: Msisitizo upo katika mstari unaofuata wa 5 ambao unasema..

Kutoka 20:5
[5]Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,


Maana yake ni kuwa, ikiwa picha hizo au sanamu hizo zinahusishwa na ibada yoyote ya rohoni, kama vile kuviabudu, au kuvisujudia au kama vile nyenzo ya ulinzi au kuombea..hayo ni machukizo makubwa sana.
Lakini kama ni picha tu, za urembo, au vinyago vya mapambo. Ikiwa ni vyema havina maudhui mabaya vimekaa tu, hakuna dhambi yoyote.


Ukizingatia kuwa hekalu la Mungu lilikuwa na michoro mingi, vilevile juu ya lile sanduku la agano wana wa Israeli waliagizwa watengeneze sanamu za makerubi.


1 Wafalme 7:29
[29]na juu ya papi zilizokuwa katikati ya vipandio kulikuwa na simba, na ng’ombe, na makerubi; na juu ya vipandio kulikuwa na tako; na chini ya simba na ng’ombe kulikuwa na masongo ya kazi ya kupembeza.
Lakini huwezi kuona mahali popote vitu hivyo vikiabudiwa au kusujudiwa.


Lakini imekuwa tofauti leo hii, baadhi ya madhehebu yanatengeneza sanamu za watakatifu wa kale kama vile Mariamu mama wa Yesu na Yosefu..na baada ya hapo wanaomba wakizipa heshima sanamu hizo kana kwamba zina jambo lolote la kiungu ndani yake.


Ikiwa wewe ni mkatoliki na sanamu hizi zipo nyumbani kwako, au picha hizo za watakatifu, ni heri ukaziondoa kwa sababu dhehebu hilo, lina mahusiano ya moja kwa moja na sanamu, kwa kuziabudu na kuzipa heshima ambazo Mungu kazikataza.


Lakini ikiwa ni picha yako tu, au ya familia au hata inayodhaniwa inafanana na ya Bwana Yesu. Ziweke tu, kama mapambo au kumbukumbu zako. Lakini usionyeshe hata chembe ya heshima kwenye hizo picha kwasababu hapana uhai wowote hapo.


Bwana ametuonya sana, juu ya ibada za sanamu. Ambazo hazipo tu katika vinyago na picha , bali mpaka kwa viumbe vyake vyote hai hadi sisi wanadamu. Usimpe yeyote heshima ya kuabudiwa isipokuwa Mungu tu peke yake muumba wa mbingu na nchi.

Vinginevyo utamtia Bwana wivu na mwisho wa siku atakuua na utakwenda jehanamu. Chukua tahadhari katika hili.


1 Yohana 5:21
[21]Watoto wadogo, JILINDENI NAFSI ZENU NA SANAMU.


Shalom.


MADA ZINGINEZO:

Kulingana na Mathayo 5:29, Je! viungo vyetu vikitukosesha tuvikate?


Bawabu ni nani na hufanya kazi gani?


Maskini wa roho ni watu wa namna gani?(Mathayo 5:3)


IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.


Je! Ni dhambi kibiblia kuwaomba wafu (watakatifu)?


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *