Kulingana na Mathayo 5:29, Je! viungo vyetu vikitukosesha tuvikate?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

“Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe;”

Tusome habari nzima;

Mathayo 5:28 “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

Maana ya kwanza ambayo Bwana alimaanisha hapo, ni kiungo kama kiungo cha mwili, mfano  jicho, mkono, mguu, sikio n.k. Ikiwa na maana ikiwa mkono wako hauwezi kuuzuia kuiba ni heri uukate, ikiwa jicho lako huwezi kulizuia kutazama mambo machafu,na uzinzi ni heri uling’oe tu, ikiwa mguu wako unakuchochoa mara kwa mara kwenda disco au kutafuta mambo yasiyompendeza Mungu, kiasi kwamba unaona kama ungekuwa mlemavu ungejiepusha na mambo mengi maovu, ni heri uukate. Na kufanya hivyo sio dhambi kabisa. Bwana ameruhusu.

Halikadhalika, vipo viungo vya rohoni, ambavyo vimeshikamana na roho zetu kiasi kwamba tukiviondoa ni lazima maumivu tupate, mfano wa viungo hivi, ni marafiki, ndugu, kazi, mazingira, n.k. Kama Ikiwa ndugu zako ndio kikwazo  cha wewe kuupokea wokovu, ni heri usifuatane nao katika mashauri yao, ili uupokee wokovu, kuliko kushikamana nao na mwisho wa siku ukapotea kuzimu wewe pamoja na wao.

Bwana Yesu alisema..

Mathayo 10:37 “Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.

Chochote kile, kiwe ni cha mwilini au cha rohoni, ukiona kinakusonga mbali na Mungu, achana nacho, kumbuka umepewa ruhusa ya kukiondoa, Hilo Mungu analiruhusu kabisa.  Yapo majira itakulazimu utumie nguvu, kuulinda wokovu wako, kwasababu dhambi nayo inatumia nguvu kukuangusha. Hivyo ukiwa legevu legevu utaupoteza uzima wako.

Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”.

Lakini swali ni je! Umeokoka? Je! Kristo akirudi leo unaouhakika kwa kwenda naye? Una habari kuwa hili ndio kanisa la mwisho, lijulikanalo kama Laodikia? Umejiwekaje tayari?

Shalom.

LEAVE A COMMENT