Bawabu ni nani na hufanya kazi gani?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Bawabu ni msimamizi wa mlangoni. Mtu anayehusika na kufunga na kufungua, aidha milango ya mji, au mahekalu au majumba ya kifalme, au maeneo ya shughuli za kazi pia ndiye anayefanya kazi za kuruhusu au kutokuruhusu vitu kuingia na kutoka getini au mlangoni.

Katika biblia vipo vifungu kadha wa kadha vinavyo wazungumzia mabawabu; Soma.

2 Samweli 18:26
[26]Kisha huyo mlinzi akaona mtu mwingine anapiga mbio; mlinzi akamwita bawabu, akasema, Angalia, mtu mwingine anakuja mbio peke yake. Mfalme akasema, Huyu naye analeta habari.


Vilevile Mordekai mjomba wake Esta alikuwa ni bawabu kwa mfalme na akafanya kazi yake kwa uaminifu mpaka sikumoja mfalme akamtukuza zaidi hata ya wafanyakazi wake wengine wenye cheo. Habari yake utaisoma katika kitabu cha Esta.


Hiyo ni kutufundisha kuwa haijalishi ni kazi ipi wewe upo, hata kama sio ya kuheshimika lakini ukiifanya kwa uaminifu Mungu atakunyanyua na kukutukuza juu hata ya wenye vyeo vikubwa zaidi yako.

Lakini Daudi anasema pia;

Zaburi 84:10
[10]Hakika siku moja katika nyua zako
Ni bora kuliko siku elfu.
Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu,
Kuliko kukaa katika hema za uovu.


Kuonyesha kuwa ni heri uifanye kazi ya Mungu ambayo ni ndogo au inayoonekana inadharaulika kuliko zote..pengine kudeki choo cha kanisa..

Kwasababu hazina yako mbinguni inadumu milele.


Kuliko kukaa katika majumba ya kifahari lakini ya waovu. Mtumikie Mungu kwa uaminifu katika kazi uliyowekwa.

Kwasababu fahamu kuwa Yesu atarudi na kumlipa kila mtu sawasawa na kazi yake ilivyo hapa duniani. Je umejiwekaje tayari?

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

Kusaga meno, ni nini kama inavyozungumziwa katika maandiko?


Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?


Je! neno “Mego” linamaana gani katika biblia?


Mwezi wa Abibu ni mwezi gani?


Mede ni nini kama tunavyosoma katika Wafilipi 3:14?


Kutabana ni nini katika maandiko? (Mika 5:12)

LEAVE A COMMENT