Mwezi wa Abibu ni mwezi gani?

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Mwezi wa Abibu.

Mwezi wa Abibu ni mwezi wa kwanza kwa Wayahudi, ambao kwetu sisi tunaotumia Kalenda ya ki-Gregory, huangukia katikati ya mwezi wa tatu (3) au Mwezi wanne (4) mwanzoni, kulingana na mwaka na mwaka.

Mwezi huu ulikuwa ni muhimu sana, kwa Wayahudi kwasababu kwanza ndio ulikuwa mwezi wao wa kutoka katika nchi ya utumwa Misri,

Kutoka 13:3 “Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa Bwana aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.

4 Ninyi mwatoka leo katika mwezi wa Abibu”.

Mwezi huu kwa jina lingine uliitwa Mwezi wa Nisani.

Katika mwezi huu walikuwa wanashehekea sikukuu kubwa tatu,

Ya kwanza ni Pasaka: Ambayo ilikuwa inafanyika kila tarehe 14 ya mwezi huo, walikuwa wanamchinjia yule mwana-kondoo na kumla bila kumsaza hadi asubuhi.

Ya pili ni Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu: Sikukuu hii ilianza mara baada ya pasaka kuisha, yaani kuanzia tarehe 15-21 ya mwezi huo huo wa kwanza. Wana wa Israeli walikuwa wakila, mikate hiyo isiyotiwa hamira, kwa hizo siku saba. Yoyote ambaye alionekana akila mkate uliotiwa chachu (yaani Hamira) aliuawa.

Ya tatu ilikuwa ni sikukuu ya mavuno/matoleo ya kwanza: Ilifanyika siku ya kwanza ya juma, katika wiki hiyo hiyo  ya mikate isiyotiwa chachu.

Sikukuu hizi zote zilimfunua Kristo Yesu, Tangu siku ile anaumega mkate na divai, kama ishara ya mwili wake na damu yake, na kama pasaka mwenyewe anayekwenda kuchinjwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Vilevile, siku ya kwanza ya Juma ndiyo aliyofufuka. Kwa maelezo marefu kuhusiana na sikukuu hizi za kiyahudi Fungua hapa>>>  https://wingulamashahidi.org/2019/06/30/sikukuu-7-za-kiyahudi-zinafunua-nini-kwetu/

Lakini Swali ni je mwezi huu Nisani/Abibu una umuhimu wowote kwetu?

Umuhimu wake upo rohoni na si mwilini, Ili Mungu atuone tumeanza mwaka wa Maisha yetu, ni sharti tumpokee Yesu Maisha mwetu, Vinginevyo haijalishi tutakuwa tumeishi miaka mingapi hapa duniani, kama Kristo bado hajazaliwa ndani yetu, bado hatuishi. Ni sawa na wafu.

Hivyo ili tuanze mwezi wa kwanza, tumpokee Yesu kama bado tulikuwa hatujampokea, na baada ya hapo, atatupa sisi uzima wake wa milele bure.

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Yesu yupo mlangoni kurudi, jiulize, Maisha yako yapo mikononi mwa nani? Yesu akirudi leo huko utakapokwenda utakuwa mgeni wa nani? Kila mmoja wetu jibu analo moyoni mwake. Yesu sio wa wakristo tu, Yesu ni wa dini zote, na yeye ndio njia, kweli na Uzima, mtu hafiki kwa Mungu, bila ya kwa njia yake yeye.

Je! Upo tayari kumpokea leo?. Kama jibu ni ndio basi fungua hapa kwa msaada wa sala ya Toba na hakika Bwana atakuokoa, katika giza hili neno lililopo sasahivi duniani. Fungua hapa >>>

https://wingulamashahidi.org/2020/07/22/kuongozwa-sala-ya-toba/

Ubarikiwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *