“Mego”, limetokana na neno, kumega.
Kitu chochote kilichomegwa, au kunyofolewa mahali Fulani, ndicho kinachoitwa “Mego”. Ni kipande kidogo katika kitu kizima.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;
Mithali 17:1 “Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi”.
Maana yake ni kuwa, ni heri kuishi katika nyumba, ambayo kinachopatikana ni kidogo, na pengine kisiwe ni kitamu au kizuri(kikavu), Kuliko kuishi katika nyumba ambayo, mnakula na kushiba, na kusaza, katika karamu lakini nyuma yake kuna magomvi, wivu, chuki, mashindano n.k.
Hii ikifunua pia maeneo mengine yote. Hata ya kazi, Ni heri ufanye kazi unayolipwa mshahara usiojitosheleza, lakini una amani nayo, haiathiri uhusiano wako na Mungu, inakupa uhuru wa ibada..Kuliko kufanyakazi zenye malipo makubwa lakini roho yako inaangamia.
Watu wengi wamekuwa wakikimbilia vitu vyenye malipo makubwa, au mwonekano mzuri, au heshima kubwa, na kusahau kuangalia nyuma ya hicho anachokitafuta kuna nini?
Herode, alikuwa ni mfalme, anayefanya karamu kubwa, lakini nyumba yake alikuwa na wivu, na chuki, na dhambi, ndio maana mke wake alimshinikiza amuue Yohana katikati ya karamu (Mathayo 14:3-11), lakini Yohana aliishi majangwani anakula nzige, na asali, lakini ndani yake ana amani na Mungu, hadi Bwana akamshuhudia kuwa hajawahi kutokea, aliye mkuu kama yeye, miongoni mwa wazao wa wanawake.
Hivyo, Bwana anatushauri, tujifunze, kuchagua jambo lenye utulivu Zaidi, kuliko lenye malipo makubwa lakini halitupi utulivu rohoni. Kwasababu vinavyotoka rohoni, kama vile utulivu, furaha, amani, upendo, vina nguvu zaidi kuliko vinavyotoka nje, kama mali, uzuri, urembo n.k.
Shalom
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Adamu na Hawa, Mungu aliwaita kwa jina moja ADAMU ?
Nondo ni kitu gani katika biblia?(Mathayo 6:19)
Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?