Je! Busu kanisani kwa watu wanaofunga ndoa ni sawa? 


SWALI: Je! Busu ni sawa mbele ya kanisa kwa watu wanaofunga ndoa (mwaume na mwanamke) kwa sababu wengi wanafanya hivyo madhabahuni wanapofungishwa ndoa? Je! Ni sahihi kufanya hivyo kanisani?


JIBU: Kabla ya kujibu swali hilo, tujiulize kwanza swali hili, je! Ni sahihi kwa wale ambao, tayari ni mke na mume kufanya kitendo hicho ndani ya kanisa? Kama si sahihi kwa watu ambao ni wana ndoa tayari kufanya kitendo hicho kanisani, basi, si sahihi pia hata kwa wale ambao wanaofungishwa ndoa kanisani, kwa sababu kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaivunjia heshima nyumba ya Mungu na madhabahu yake.


Kitu kisicho fahamika na wengi ni kuwa, kanisa ni nyumba takatifu ya Mungu, kanisa ni sehemu ya kumwabudu Mungu, na panapaswa kuheshimiwa, hivyo, vitendo vyovyote visivyo mpa Mungu Utukufu kama, kucheza kwa kuruka sarakasi madhabahuni, kukata viuno madhabahuni, na kitendo hicho cha busu madhabahuni havitakiwi kabisa katika nyumba ya Bwana, na wala si kanisani tu, bali sehemu yoyote ile ya wazi, ninyi kama wana ndoa wa kikristo,  si sahihi kwenu kufanya hivyo hata kidogo. Hamuwezi fanya hicho kitendo mkiwa mbele ya watu sokoni au Kwenye kituo cha magari, au barabarani mbele za watu, huko ni kukosa na kukoseana heshima kati ya mke na mume, huo ni uzinzi na uasherati ambao hauna utofauti na watu wasio na Roho mtakatifu wanao ufanya huo uchafu. 

Biblia inasema ndoa na iheshimiwe na watu wote.

Waebrania 13:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 

Sherehe yenu au tafrija yenu haiwezi badili hilo andiko, hicho kitendo kifanyike sehemu husika na watu husika (yaani mke na mume na sio boyfriend na girlfriend) na wala si madhabahuni pa Mungu. 

Shea na wengine ujumbe huu

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312


MADA ZINGINEZO:

Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.


JE! NI LAZIMA TUNAPOSALI TUPIGE MAGOTI?


BWANA ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA “HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU?”


ALIKUWA HAMJUI BWANA BADO, NA NENO LA BWANA LILIKUWA BADO HALIJAFUNULIWA KWAKE.

One Reply to “Je! Busu kanisani kwa watu wanaofunga ndoa ni sawa? ”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *