Kwanini Adamu na Hawa, Mungu aliwaita kwa jina moja ADAMU ?

Jibu: Tusome..

Mwanzo 5:1 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki AKAWAITA JINA LAO ADAMU, siku ile walipoumbwa”.

Sio kwamba, Mungu alikosea, kuwapa jina moja, kana kwamba hakumuona mwanamke Hawa.

Hapana, kulikuwa na sababu kubwa sana.. Mungu anavyoona sio kama sisi tunavyoona. Sisi tunaona ni watu wawili tofauti, lakini Mungu alikuwa anawaona ni mtu mmoja, na hivyo wamestahili jina lile lile moja, alilowapa tangu mwanzo yaani Adamu.

Kwasababu mwanamke alitoka katika ubavu wa Adamu, hivyo ni yuleyule Adamu tu.

Lakini ujumbe gani, Mungu anapitisha?

Kwanza, ni kuonyesha kuwa mke na mume, mbele za Mungu ni mtu mmoja. Kwasababu Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hivyo, baraka na laana wote wanashiriki kwa Pamoja. Mtu yeyote anayeingia katika ndoa hapaswi kumwona mwezi wake kama mtu baki, bali kama sehemu ya mwili wake kabisa. Hivyo anawajibu wa kumtunza na kumtimizia mahitaji yake yote. Ukifanya kinyume na hapo, ujue unakwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

1Wakorintho 7:4 “Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe”.

Wapo wanaume wanaowaona wanawake, kama vyombo tu vya starehe na si zaidi, na kusahau kuwa wanakiuka kanuni ya wawili kuwa kitu kimoja.

Pili, ni kwamba, mwanamke anapaswa amtii mume wake. Kwasababu haitwi tena kwa jina lake bali kwa jina la mumewe..Watu wengi hawajui utaratibu wa majina ya mwisho ya wazazi au ya wake kwanini yanakuwa ya mwanamume. Utaratibu huo haukuanzia kwa mwanadamu, kama wengi wanavyodhani wakisema ni mfumo dume, hapana. Bali uliwekwa na Mungu mwenyewe. Alimuitwa mwanamke kwa jina la mumewe Adamu.

Kufunua nini? Kufunua kuwa mwanamke anapaswa atii, kwa kila namna, na kukubali kuongozwa na mwanaume. Ikiwa wewe umeolewa, fahamu kuwa kichwa chako ni mumeo, na kichwa na mumeo ni Kristo. Hivyo unawajibu wa kutii, ndivyo Mungu alivyoagiza.

Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa, ndoa ina siri kubwa nyuma yake. Na siri yenyewe ndio hiyo ya kugeuzwa na kuwa mwili mmoja. Ikifunua Kristo na kanisa lake.

Biblia inasema..

Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Bwana akubariki

Mada Nyinginezo:

NAO WATAJIEPUSHA WASISIKIE YALIYO KWELI

Nondo ni kitu gani katika biblia?(Mathayo 6:19)

JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA MITUME ANDREA NA FILIPO.

Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)

Rudi Nyumbani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *