Ni tabia ipi ya Uungu tutakayoshiriki (kulingana na 2 Petro 1:4)

  Mungu, Uncategorized

SWALI:    2 Petro 1:4 inasema…

2 Petro 1:4 

Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo MPATE KUWA WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. 

Sasa ni tabia ipi iyo ya Uungu tutakayokuwa washirika wake?

JIBU:  Tabia ya Uungu tutakayoshiriki ni ile ya mwili wa Utukufu wa Bwana wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo,

2 Wathesalonike 2:14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ILI KUUPATA UTUKUFU WA BWANA WETU YESU KRISTO. 

ambayo katika hiyo tutaishi milele pasipo kufa wala kuugua na kutawala naye hapa duniani baada ya karamu ya Mwana-Kondoo na yeye akiwa kama Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Na tabia hiyo tutaitoa kutoka kwake kwenye ile siku ijulikanayo kama unyakuo, ambapo miili yetu itabadilika kwa kufumba na kufumbua na kisha kufanana na yeye kama mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi yaani wale wamwaminio.

Warumi 8:29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili WAFANANISHWE NA MFANO WA MWANA WAKE, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 

Na ni Kristo Mwenyewe ndiye atakaye tubadilisha miili yetu hii ya unyonge na kutuvisha ule mwili wa Utukufu unao fanana na yeye 

Wafilipi 3:20  Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; 

21 ATAKAYEUBADILI MWILI WETU WA  UNYONGE, UPATE KUFANANA NA MWILI WAKE WA UTUKUFU, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake. 

Ambapo katika miili hiyo ya Utukufu Mkuu na wa ajabu na ya uzuri usioelezeka, hakutokuwa na kuoa wala kuolewa sawasawa na (Luka 20:35) bali tutafanana na Bwana kwa Utukufu na kung’aa kama nyota za Mbinguni milele na milele 

Danieli 12:3 Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele. 

Lakini hatutakuwa na utukufu unao fanana, maana kuna utofauti wa fahari pia kati nyota na nyota, na pia upo utofauti wa fahari kati ya jua na mwezi, ndivyo itakavyokuwa na huko pia katika ufalme wa Mungu utakao simama milele na milele, kutakuwa na utofauti kutokana na kazi zetu tulizozifanya katika Bwana, lakini sote tutafanana naye.

1 Wakorinto 15:41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.

Hivyo ndugu yangu uliye katika Bwana, endelea kumtumikia Mungu kwa nguvu zote kwa kadiri ya neema uliyojaaliwa huku ukitembea katika utakatifu na na kujitakasa kila dakika.

1 Yohana 3:2  Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 

3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312



MADA ZINGINEZO

ONDOENI MIUNGU MIGENI ILIYO KWENU.


Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)


Omri ni nani kwenye maandiko na sheria zake ni zipi? (Mika 6:16)


DAMU YAKE NA IWE JUU YETU.

LEAVE A COMMENT