Nondo ni kitu gani katika biblia?(Mathayo 6:19)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utaweza kukutana na Neno hilo.

Isaya 51:7 “Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao.

8 Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote”.

Mathayo 6:19 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;”

Soma pia, Ayubu 4:19, Zaburi 39:11, Yakobo 5:1,

Swali ni je! Nondo ni kitu gani?

Nondo ni wadudu jamii ya vipepeo, ambao kwa asili wanapokaribia wakati wa kutaga mayai yao, huwa wanapendelea mazingira ya nyumba za watu, hivyo huingia ndani na kwenda kutaga mayai yao sehemu zenye manyoya au pamba pamba, kama vile makapeti au mapazia n.k..

Na lengo la kufanya hivyo ni ili Watoto wao, wanapozaliwa wapate sehemu ya kupata chakula.. kwasababu manyoya au pamba ndio chakula chao.

Hivyo, Watoto wanapoanguliwa, ndipo nguo zinapoanza kutafunwa. Utashangaa, ulinunua gauni lako zuri, ukaliweka kabatini, lakini baada ya wiki kadhaa unakuta matobo kwenye gauni hilo, unajiuliza matobo haya yametoka wapi?

Hiyo inafunua nini?

Bwana Yesu alisema, tusijiwekee hazina duniani ambamo kuna nondo.. Maana yake ni kuwa hazina zetu, zitakutana na waharibifu, endapo tutaziwekeza sehemu isiyosahihi.

Ikiwa tunachokipata chote, ni kuwekeza tu duniani, hatuwekezi kwa Mungu, siku moja tutakufa na hizo mali zisitusaidie, au zitaibiwa, au zitatumiwa katika matatizo n.k. Lakini tukiwekeza kwa Mungu, uhakika tunao wa thawabu yetu milele mbinguni. Utalipwa siku ile utakapokwenda mbinguni.

Inasikitisha kuona watu wengi, hawaijali injili hata kwa mali zao. Ndugu ikiwa huwezi kuwa mhubiri, basi sapoti injili kwa ulichojaliwa. Ili uwe umeifanya kazi ya Mungu kwa njia hiyo. Jitoe kwa maendeleo ya kanisa la Kristo, na watakatifu wake, ni muhimu sana, jiwekee hazina mbinguni.

Lakini kama itakuwa wewe unachowaza ni kujilimbikizia tu, fahamu kuwa nondo na kutu, vipo karibu nawe, kula kila unachokisumbukia.

Bwana atusaidie.

Ikiwa hujampa Yesu Kristo Maisha yako, huna sababu ya kuendelea kubaki katika hali hiyo hadi sasa. Kumbuka siku yoyote ni parapanda, jiulize, Yesu akirudi leo utamwambia nini, au ukifa katika dhambi utakuwa mgeni wa nani huko uendako?

Ikiwa upo tayari kuokoka, basi bofya hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya toba, >>> SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)

Ufisadi ni nini katika maandiko?(Waefeso 5:18)

INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI

Rudi Nyumbani

LEAVE A COMMENT