Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Nini maana ya mstari huu? “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako” mathayo 6:2

JIBU: Tosome huo mstari

Matayo 6:2  BASI WEWE UTOAPO SADAKA, USIPIGE PANDA MBELE YAKO, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu

Panda ni pembe ya kondoo mume, ambayo ilitumika zamani kama tarumbeta. ( tazama picha )

Panda Ilipopigwa iliashiria aidha kutangaza jambo jipya na kutoa tahadhari. Pia ilitumika kutangaza vita n.k

 Bwana Yesu aliposema tusipige panda mbele yetu tutoapo sadaka alimaanisha kuwa, hutakiwi kuanza kutoa taarifa au kutangaza kwa watu huko na huko kuwa sasa naenda kutoa sadaka au sasa naenda kutoa msaada mahari fulani, mambo kama hayo hufanywa na wanafki huko na huko ili watukuzwe na watu, baadhi ya watu wanapotaka kupeleka msaada kwa watu wasiojiweza ama walemavu au watoto yatima, utakuta mtu kama huyo anatangaza kwenye vyombo vya habari kama television magazeti n.k na lengo la kufanya hivyo ni ili atukuzwe na watu. 

Sasa watu kama hao Bwana anasema wamekwisha kupata twawabu za huo unafki wao (yaani hakuna walichofanya mbele za Mungu). Lakini sisi Wakristo hatutakiwi kufanya hivyo, hatutakiwi kwenda huko na huko kutangaza kwenye matalevisheni na magazeti kuwa napeleka sadaka au msaada ili tutazamwe na watu, kwani tukifanya hivyo hatutopata thawabu yoyote ile

Matayo 6:1  ANGALIENI MSIFANYE WEMA WENU MACHONI PA WATU, KUSUDI MTAZAMWE NA WAO; kwa maana mkifanya kama hayo, HAMPATI THAWABU KWA BABA YENU ALIYE MBINGUNI. 

Hivyo mkristo utoapo sadaka au msaada, huna haja ya kutangaza huko na huko ili upewe utukufu na watu, bali toa sadaka yako au msaada kwa kwa guswa kabisa kutoka moyoni, ama kwa kuchangia kazi ya Mungu au kusaidia wasiojiweza na Mungu atakujaza.

Lakini kama bado hujafanyika kuwa mkristo na upo nje ya wokovu, amua leo ndani yako kumpokea Yesu kwani tunaishi nyakati mbaya mno. Unachotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako ndani ya moyo wako kwa kudhamiria kuziacha, kama ni uzinzi, ulevi, uvaaji suruali na vimini kwa wanake make up n.k kisha tafuta ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo sawa sawa na matendo 10:48

Bwana akubariki. shalom.


MADA ZINGINEZO

Mede ni nini kama tunavyosoma katika Wafilipi 3:14?


Bawabu ni nani na hufanya kazi gani?


Lumbwi ni kiumbe gani kwenye maandiko?

LEAVE A COMMENT