Lumbwi ni kiumbe gani kwenye maandiko?

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Lumbwi kwa jina lingine ndio KINYONGA. Wengi wetu tunamfahamu kama mnyama ambaye anatabia ya kubadilika rangi kulingana na mazingira..

Katika biblia anatajwa kama mmoja wa wanyama najisi, asiyeliwa .

Mambo ya Walawi 11:29-30
[29]Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake,
[30]na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi.

Hata mizoga yao haikuruhusiwa kuguswa.

Lakini ni kwanini, katika agano la lake Mungu aliwabagua wanyama na kuwaweka katika makundi hayo mawili yaani “najisi na wasio najisi”?

Ni kwasababu ya tabia zao walizonazo..ambazo hata sasa baadhi ya watu wanazo rohoni na hivyo, Mungu anawaona kama vile ni najisi.

Na tabia zenyewe ndio kama hizi za lumbwi / kinyonga..ambao hawana taswira moja..bali wanajigeuza geuza yaani utakuta leo mtu anaenda kanisani anamsifu Mungu kweli katika Roho, lakini kesho akitoka akienda kwenye sherehe fulani ataruka ruka na kuimba nyimbo za kidunia kama vile sio yule aliyekuwa anamsifu Mungu jana.

Au mwingine leo anavaa vizuri kisa tu anakwenda kanisani..akitoka baadaye anabadilisha mavazi anavaa vimini na suruali, anakwenda kazini..kiasi kwamba hata mtu akimtazama hawezi kusema huyu ni mtu anayemjua Mungu. Lakini muda huo huo anasifika kanisani kama binti anayejua kuvaa vizuri na kujisitiri..

Sasa hawa ndio wakina lumbwi, ambao mbele za Mungu ni najisi..Mungu amewakataa, kwa jina lingine ni watu vuguvugu, ambao Bwana Yesu amesema atawatapika watoke katika kinywa chake..

Ufunuo wa Yohana 3:15-17
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Ndugu unajisikiaje kufanana na Lumbwi? Ni heri umgeukie Kristo kwa kumaanisha akuokoe ili unafki uondoke ndani yako kisha akujaze Roho wake Mtakatifu uwe hai rohoni.

Hizi ni siku za mwisho na Bwana Yesu yupo mlangoni kurudi..tubu mgeukie Bwana akusaidie. Ikiwa upo tayari kumpa leo Yesu maisha yako kwa kumaanisha kabisa..Basi fuatiliza sala hii ya Toba kwa kufungua hapa >>>

Maranatha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *