Naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Bwana Yesu alikuwa na maana gani kusema..

“naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki”.

Tusome:

Mathayo 21:42-44
[42]Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu?
[43]Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
[44]Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.

Ukianzia hapo juu utaona Bwana Yesu anajifananisha na lile jiwe kuu la waashi( yaani wajenzi)…ambao zamani katika ujenzi wao wa majumba makubwa ilikiwa ni lazima jiwe hilo la pembeni liwekwe kama sapoti ya jengo lote..kiasi kwamba ukijenga nyumba bila ya kuliweka jiwe hilo ambalo lilikuwa linakaa kwenye pembe ya nyumba basi ni sawa na kujenga nyumba pasipo kuweka msingi..

Hivyo katika habari hiyo anajielezea yeye kama ndio hilo jiwe la pembeni ambalo mwanzoni wajenzi waliliona halifai pengine ni bovu, lakini baadaye wakagundua kuwa lilikuwa imara sana lingewafaa sana..

Ndio hapo anasema..Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;

Ikifunua kuwa Bwana Yesu ni Jiwe muhimu sana katika ujenzi wa maisha yetu, ya hapa duniani na kule ng’ambo tutakapofika..tukimtupa nje leo siku zitafika tutagundua kuwa uamuzi tulioufanya zamani haukuwa mzuri..

Lakini hiyo ni sehemu ya kwanza ya sifa ya jiwe hilo kwamba ni la muhimu katika ujenzi wa maisha yetu..

Sehemu ya pili ni kuwa jiwe hilo lina tabia yake ya kipekee embu tuisome tena…

“Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki”

Maneno hayo yanatuonyesha kuwa jiwe hilo ni GUMU sana na ndio maana anasema atakayeanguka juu yake atavunjika vunjika..lingekuwa ni jiwe la udongo, angeumia tu asingevunjika, lakini kwasababu ni gumu ndio maana lazima uvunjike..

Halikadhalika anasema jiwe hilo litakayemwangukia litamsaga tikitiki..kuonyesha kuwa ni kubwa na zito..ndio maana lina uwezo wa kumsaga mtu tikitiki.

Akifunua kuwa kwa yeyote atakayejaribu kwenda kinyume na Kristo, atakayempinga ni anajitafutia tu uharibifu wake mwenyewe usioponyeka..Kama vile hapo alivyokuwa anawalenga wale wakuu wa makuhani na wazee, waliofuata kumtega.

Ambao walikuwa wanatafuta namna ya kumuua ndipo akawapa mfano huo.

Hata sasa watu hawajui thamani ya jiwe hili, ndio maana wanaishi maisha wanayotaka, wanadhani maisha yao yanajengwa na fedha tu, na sio Mungu..na wengine wanakwenda mbali zaidi kufikia hatua ya kuipinga injili..hawa hali yao ndio mbaya zaidi kwasababu ni aidha wataliangukia jiwe hilo, au litawaangukia wao na kusiwe na kuponyeka.

Lakini ni heri ukajenga juu ya JIWE hili gumu uwe salama..kama alivyosema katika.

Mathayo 7:26-27
[26]Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
[27]mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Swali ni je! Yesu ni nani kwako? Je tayari ameshafanyika kuwa Bwana na mwokozi na kiongozi wa maisha yako? Kumbuka hakuna njia nyingine yoyote ya kumfikia Mungu zaidi ya Yesu Kristo Bwana wetu.

Hivyo kama upo tayari leo kutubu basi fungua link hii… Au wasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312/ +255693036618.

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT