Kutahayari ni nini katika biblia?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

JIBU: neno kutahayari tunaweza lisoma katika vifungu hivi.

Yeremia 6:15   Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajilia wataangushwa chini, asema Bwana. 

Tunaweza soma tena katika 

Yoeli 2:27   Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe. 

Unaweza pitia pia kwa muda wako

Luka 13:17.  Warumi 10:11. Isaya 1:29. Zaburi 83:17

Kutahayari maana yake ni kuogopa kwa kuona aibu au kuwa na hofu kwa kuona aibu. Wakristo wengi leo hii wanashindwa kumkiri Bwana Yesu katika maisha yao kwa kuona aibu wakifikiri kuwa watu watawaonaje? Lakini hii ni mbaya sana kwani Bwana na yeye atatuonea aibu mbele ya malaika wa Mbinguni siku ile.  Kama Bwana Yesu hakutahayari siku ile aliyoenda kusurubiwa msalabani inatupasaje sisi? Bwana aliishinda aibu pale msalabani kwaajiri yetu, sasa inatupasaje sisi? 

Mtume Paulo alisema maneno fulani katika 

2 Timotheo 1:12   Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile. 

Alisema kuwa kwasababu ya Bwana Yesu haoni aibu kwani anafahamu jinsi alivyomwaminifu. 

Je! Na wewe unatahayari linapokuja suala la kuwahubiria wengine habari njema za wokovu? Unatahayari linapokuja suala la kuthibitisha imani yako kwa Bwana Yesu katikati ya walevi, waasherati, waabudu sanamu n.k ndugu yangu huna sababu ya kufanya hivyo jua Bwana Yesu ni mwaminifu na yeye mwenyewe alisema kuwa tujipe moyo kwani hata yeye aliyashinda yote wala hakutahayari lilipokuja suala la kuwafundisha wengine, wala hakutahayari lilipokuja suala la kuwahubiri wengine, vivyo hivyo na sisi tumfuate Kiongozi wetu Yesu Kristo pasipo kutahayari kama maandiko yanavyosema katika 

2 Timotheo 2:15   Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. 

Bwana akubariki. Shalom 


Mada zinginezo:

Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?


Lumbwi ni kiumbe gani kwenye maandiko?


Usimkatae (usimwache) Yesu aliye tumboni mwa Mariamu!


MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.


Mwezi wa Abibu ni mwezi gani?


Kusaga meno, ni nini kama inavyozungumziwa katika maandiko?

LEAVE A COMMENT