MWANAMKE ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE, JE!  NI UZAZI UPI HUO UNAOZUNGUMZIWA?

SWALI: Biblia inasema katika (1 Timotheo 2:15) kuwa, Mwanamke ataokolewa kwa uzazi wake, je! Ni uzazi upi huo unaozungumziwa?


JIBU:  Tusome…

1 Timotheo 2:12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

 14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

15 WALAKINI ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi. 

Maneno hayo yanakuja baada ya mtu wa Mungu Paulo kuelezea zuio la mwanamke kuhubiri kanisani, na sababu ya msingi aliyoitoa ni udhaifu wa mwanamke katika kudanganyika kirahisi, Adamu hakudanganyika bali Hawa, na akauuza UZAZI wake chini ya dhambi hali ambayo kila mtu leo anamtaja hawa si kwa sifa nzuri ya kutuzaa bali ile mbaya ya kutenda dhambi. Ni kweli kwamba, kupitia yeye uovu ukazaliwa na tangu wakati huo mauti ikatawala kwa watu wote kwa sababu wote tumetenda dhambi. 

Hakupatikana mkombozi mwenye ujuzi wa kweli uletao uzima wa kuondoa kosa lake au kukomboa uzazi wake, (hata Adamu mwenyewe alikomboa nafsi yake tu, hajui hatima ya watoto wake aliowazaa)

Lakini pamoja na kukosa huko, Paulo anasema “mwanamke huyo atakombelewa kupitia uzazi wake yeye mwenyewe” Sasa, uzazi wake huo ni upi?..

Wagalatia 4:3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe AMBAYE AMEZALIWA NA MWANAMKE, amezaliwa chini ya sheria

Unaona hapo ni uzazi  wa mwanamke ulioleta ukombozi na kututoa chini ya sheria na ile laana ya kosa la kwanza la mama yetu Hawa.. Na uzao wake ulioleta ukombozi si mwingine bali ni Mwana wa Adamu aitwae Yesu Kristo, aliyezaliwa na Mariamu pasipo baba wa kimwili, huyo ndiye uliyekuja kuukomboa uzazi wa Hawa, alileta njia ya kweli na uzima na lile kosa la Hawa ambalo liliutia ulimwengu giza kwa ule ujuzi wa mabaya likashindwa mbele zake na hatimaye kumekuwa nuru kama alivyosema..

Yohana 12:46 MIMI NIMEKUJA ILI NIWE NURU YA ULIMWENGU, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

Lakini hapo sio wote wanakombolewa kutoka katika kukosa lile, bali wale ambao watamtii Yesu Kristo…

Mtume Paulo alimaliza kwa kusisitiza hilo

1 Timotheo 2:15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika IMANI NA UPENDO NA UTAKASO, PAMOJA NA MOYO WA KIASI.

Hivyo, ikiwa  mwanamke na watoto wake, watadumu katika imani ya kumwamini Yesu, na Upendo na utakaso kwa Roho wake mtakatifu, na moyo wa kiasi, ataokolewa kwa uzazi wake.

Hivyo, uzazi uliozungumziwa hapo ni Yesu Kristo, na kama bado hujamwamini mwamini sasa kwa sababu yu karibu kurudi na kuchukua walio wake, wale walio na JUHUDI KATIKA UJUZI WA KWELI ILE ILETAYO UTAUWA (Tito 2:14), na kisha kuuadhibu ulimwengu kwa maovu yake. 

HAUTAMDINGIZIA HAWA, MAANA UMEPEWA MKOMBOZI AMBAYE NI YESU KRISTO.

Bwana akubariki, Shalom.

Maran atha!

+255755251999/ +255652274252



Mada zinginezo:

IFAHAMU HUDUMA YA MWANAMKE “MZEE “KATIKA KANISA.


Kwanini biblia inalitambua kanisa kama mwanamke?


Kwanini Adamu na Hawa, Mungu aliwaita kwa jina moja ADAMU ?


 Je! Ni lazima mgonjwa adongoke chini pale anapoombewa?


Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?

2 thoughts on - MWANAMKE ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE, JE!  NI UZAZI UPI HUO UNAOZUNGUMZIWA?
  1. It is perfect time to make some plans for the future and
    it is time to be happy. I’ve read this post and if I could I want to suggest you some interesting things
    or suggestions. Perhaps you can write next articles
    referring to this article. I wish to read even more things
    about it!

    my blog post; website here – Rebbeca,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *