Kiti cha enzi cha joka kilipo ni wapi?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Swali: ufunuo 13:2 inasema…

Ufunuo 13:2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka AKAMPA NGUVU ZAKE NA KITI CHAKE CHA ENZI NA UWEZO MWINGI.   

Je! Kiti cha enzi cha joka kilipo ni wapi, na ni nani atakayepewa kiti cha enzi na nguvu?

JIBU: Kiti cha enzi cha joka (ibilisi na shetani) kinachozungumziwa hapo ambacho mnyama atapewa na huyo joka ni hapa hapa duniani kwa sababu ibilisi ndio mkuu wa dunia hii ( lakini ni kwa kitambo tu)

2 Wakorinto 4:3 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 

4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 

Joka (ibilisi) atampa mnyama mamlaka yote ya dunia juu ya watu wote watakaobaki baada ya kanisa la Kristo kuondoka ili kufanya kazi ya kuudanganya ulimwengu, na  mnyama atakayepewa huo uwezo na mamlaka sio mnyama halisi ila ni binadamu na tena ni mwamume na atatoka katika kiti cha upapa katika kanisa katoliki, huyo ndiye atakayepewa mamlaka juu ya watu wote baada ya kanisa la Kristo kunyakuliwa.

Kama vile Mungu ambaye ni Roho (Yohana 4:24) alivyojidhihirisha katika mwili (kama Kristo) kwa kazi ya ukombozi wa wanadamu na dhambi ili waingie katika uzima wa milele, ndivyo itakavyokuwa na kwa shetani pia ambaye ni roho (kwa sababu shetani alikuwa malaika na malaika ni roho), atakavyo jidhihirisha katika mwili (kama mpinga Kristo) kwa ajili ya uharibifu wa wanadamu ili waingie katika maangamizi ya milele.

Bwana Yesu alimtabiri huyo kwa kusema..

Yohana 5:43  Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; MWINGINE AKIJA KWA JINA LAKE MWENYEWE, MTAMPOKEA HUYO.

Huyo mwengine atakayekuja kwa jina lake ndiye huyo mpinga Kristo, ambaye ukishindwa kumpokea Kristo sasa utampokea huyo tu kwa sababu biblia inasema ana KINYWA CHA SIMBA (kufunua kuwa, maneno yake ni yenye mamlaka na ushawishi lakini ni ya makufuru na yaliyo kinyume na Maandiko ya Mungu), na ndio maana si ajabu leo hii kuona baadhi ya viongozi wanafki (wapenda fedha na madaraka), wanashindwa kusimama katika kweli ya Mungu wakikubaliana na kunyamazia maneno ya makufuru yanayotolewa na kiongozi huyo kama vile kukubali ndoa za jinsia moja nje ya kanisa badala ya kuyakema matendo hayo ya giza kama biblia ilivyoagiza..

Waefeso 5:11  Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, BALI MYAKEMEE; 

Hivyo, ukishindwa kumpokea Kristo leo hii,  basi tambua kuwa, utampokea na kumkubali huyo mpinga Kristo, wala hakuna kuwa katikati. Na endapo utakufa leo ukiwa ni mwomba wafu na msujudia masanamu, au kukubaliana na mafundisho yoyote ya kanisa katoliki yaliyo kinyume na neno la Mungu, safari yako ni moja kwa moja Jehanamu ya moto kama usipotaka kutoka huko na kuigeukia injili iliyohubiriwa na mitume wa Bwana.


Kumbuka, atakuwa na mamlaka juu ya wanadamu wote na kuwadanganya, kwa kuwashawishi kuipokea chapa yake na kuwaua wote watakao kataa, hatojali cheo chako na umaarufu wako, wadhifa wako na ukuu wako, nguvu zako na uhodari wako, utajiri wako na ufukara wako, urembo wako na uzuri wako,  elimu yako na ujinga wako, yeye kazi yake itakuwa ni moja tu, kukudanganya ili utupwe kwenye moto wa milele. Hivyo, jiokoe nafsi yako sasa kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina  Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ili Bwana ajapo ukamlaki mawinguni.

Bwana akubariki, Shalom.

+255755251999/ +255652274252


Mada zinginezo:

Waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 

DUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME.


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


NIFANYE NINI KAMA MKRISTO ILI MUNGU ANIONGEZEE IMANI KWAKE?


Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?

One Reply to “Kiti cha enzi cha joka kilipo ni wapi?”

LEAVE A COMMENT