TABIA YA YEHOYAKIMU INAYOENDELEA SASA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Hii ni tabia ya Yehoyakimu aliyekuwa mfalme wa Yuda ambayo inaendelea sasa katika nyakati hizi za mwisho, tabia ambayo wewe ndugu mpendwa unayesoma ujumbe huu hupaswi kuwa nayo na unapaswa kujiepusha nayo gharama yo yote ile. Na tabia Yenyewe ni ile ya kudhihaki na kumfanyia jeuri Mungu Muumba wa mbingu na nchi pale ambapo anatuhurumia sisi watenda dhambi (kutokana uovu alioukusudia juu ya wote wasio mcha Yeye), kwa kututaka tugeuke katika njia zetu mbaya ili kusudi atusamehe maovu yetu yote kama alivyosema katika.

Ezekieli 18:21 Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. 

22 DHAMBI ZAKE ZOTE ALIZOZITENDA HAZITAKUMBUKWA JUU YAKE HATA MOJAWAPO; katika haki yake aliyoitenda ataishi. 

23 Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? 

Lakini kwa tabia ya Yehoyakimu ambayo inayoendelea sasa miongoni mwa watu katika nyakati hizi za mwisho ni kinyume chake, yenyewe ni kudhihaki maonyo ya Mungu na kutenda mambo ya jeuri (ndivyo alivyofanya Yehoyakimu mfalme wa Yuda).


Biblia inasema kuwa, Mungu aliwahurumia nyumba ya Yuda (kutokana na mabaya aliyokusudia kuwatenda), hivyo, akamwambia nabii Yeremia kuyaandika maneno yote ambayo Yeye Mungu alimwambia nabii Yeremia juu ya Yuda na juu ya mataifa yote, huenda basi, watu hao watatubu ili Mungu awasamehe maovu yao.

Yeremia 36:1 Ikawa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, 

2 TWAA GOMBO LA CHUOUKAANDIKE NDANI YAKE MANENO YOTE NILIYOKUAMBIA JUU YA ISRAELINA JUU YA YUDANA JUU YA MATAIFA YOTE, tangu siku ile niliponena nawe, tangu siku za Yosia, hata siku hii ya leo. 

HUENDA NYUMBA YA YUDA WATASIKIA MABAYA YOTE NILIYOKUSUDIA KUWATENDAWAPATE KURUDI, KILA MTU AKAIACHE NJIA YAKE MBAYA; nami nikawasamehe uovu wao na dhambi yao. 

Na Yeremia akafanya Kama alivyoagizwa na Bwana kwa kumwambia Baruku kuyaandika maneno yote yaliyotoka katika kinywa chake Yeremia na kisha kwenda kuyasoma maneno hayo ya ghadhabu kwa watu hao wa Yuda.

Yeremia 36:4 Kisha Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; naye Baruku akaandika katika gombo la chuo maneno yote ya Bwana, yaliyotoka kinywani mwa Yeremia, ambayo Bwana amemwambia. 

5 Yeremia akamwagiza Baruku, ya kwamba, Mimi nimefungwa, siwezi kuingia katika nyumba ya Bwana. 

6 Basi, enenda wewe, ukasome katika gombo la chuo, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya Bwana yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya Bwana, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda, watokao katika miji yao. 

7 Labda wataomba dua zao mbele za Bwana, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; KWA MAANA HASIRA NA GHADHABU NI KUU SANAALIZOTAMKA BWANA JUU YA WATU HAWA

(Kwa undani wa habari hiyo, unaweza soma kitabu cha Yeremia sura yote ya 36).


Lakini maneno hayo ya ghadhabu ya Mungu (maonyo ya Mungu), yaliyoandikwa katika Gombo la chuo, yenye lengo la kuwataka Watu watubu na kugeuka katika njia zao, pindi tu yalipomfikia Yehoyakimu mfalme wa Yuda (kwa kusomwa mbele zake na mbele za watumishi wake), Yehoyakimu alifanya dhihaka na jeuri, kwa kulichoma lile gombo la chuo katika moto, na kibaya zaidi hakuogopa, yeye wala watumishi wake kwa kurarua mavazi yao, tofauti kabisa na Yosia baba yake (1 Nyakati 34:19).

Yeremia 36:21 Basi, mfalme akamtuma Yehudi aende akalilete lile gombo; naye akalitoa katika chumba cha Elishama, mwandishi. YEHUDI AKALISOMA MASIKIONI MWA MFALMENA MASIKIONI MWA WAKUU WALIOSIMAMA MBELE YA MFALME

22 Basi mfalme alikuwa ameketi katika nyumba iliyotumika wakati wa baridi, mwezi wa kenda; na pale PALIKUWA NA MOTO WA MAKAA MBELE YAKE

23 Hata ikawa, YEHUDI ALIPOKUWA AMEKWISHA KUSOMA KURASA TATU NNEMFALME AKALIKATA KWA KIJEMBEAKALITUPA KATIKA MOTO WA MAKAAHATA GOMBO LOTE LIKAWA LIMEKWISHA KUTEKETEA KATIKA HUO MOTO WA MAKAA

24 Lakini hawakuogopa, wala hawakurarua mavazi yao, wala mfalme, wala watumishi wake hata mmoja waliosikia maneno hayo yote. 

Hivyo ndivyo Mfalme Yehoyakimu alivyoyadhihaki maonyo ya Mungu yaliyomtaka amgeukia Mungu kwa faida yake yeye mwenyewe (Hii inahudhunisha sana). 


Lakini kilichompata Yohoyakimu kutokana na dhihaka yake hiyo kwa maonyo ya Mungu, hadi leo hii tunakisoma katika maandiko (kwa kuwa Mungu hadhiakiwi), Yehoyakimu alikufa kifo cha aibu sana kama mfalme, kwa kuwa hakuna aliyemwombolezea Yehoyakimu, bali alizikwa KWA MAZIKO YA PUNDA, akibururwa mchana kweupe na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.

Yeremia 22:18 Basi, Bwana asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake. 

19 ATAZIKWA MAZIKO YA PUNDA, AKIBURURWANA KUTUPWA NJE YA MALANGO YA YERUSALEMU.

Soma tena

Yeremia 36:30 Basi, Bwana aseme hivi, katika habari za Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; NA MZOGA WAKE UTATUPWA NJE WAKATI WA MCHANA UPIGWE KWA HARINA WAKATI WA USIKU UPIGWE KWA BARIDI

Sasa tabia hii ya Yehoyakimu ya kudhihaki na kudharau maonyo ya Mungu yanayotutaka tutubu na kumgeukia Mungu kwa faida zetu wenyewe, ndiyo inayoendelea sasa katika nyakati hizi za mwisho, unapewa ujumbe wa maonyo ya Mungu kwenye kipeperushi unaokutaka umgeukia Mungu, ndio kwanza unadharau kwa kwenda kufungia kipeperushi hicho maandazi, au unakichana kwa kukikanyaga chini na kukitupa kwenye mtaro.


Kwaa sababu wewe ni binti kijana, basi unadharau na kudhihaki jumbe za Mungu zinazokukataza kuvaa yasiyo ya adiri, na tena, unawadhihaki mabinti wasio vaa nusu uchi, vimini, suruali na kuwaona washamba, wamepitwa na wakati (wanajizeesha)


Kwa sababu una cheo fulani au elimu fulani, basi unawadhihaki wanaokuletea ujumbe wa Mungu kwa kukwambia tubu na kuitii injili, unaanza kusema ni njaa zinawasumbua hawa, wamekosa kitu cha kufanya, hawana kazi ya kufanya.


Kwa sababu una afya, una kazi, una pumzi na nguvu, basi unadhihaki maonyo ya Mungu yanayokwambia kuabudu sanamu na kuomba wafu ni dhambi, miziki ya kidunia na anasa ni dhambi, unadhihaki kwa kusema wewe ndio mkristo peke yako? Umechanganyikiwa wewe, umerukwa na akili, umelogwa wewe, na dhihaka nyingine nyingi unazozifanya pale unapoletewa maonyo ya Mungu kwa njia mbali mbali, 


Ndugu mpendwa, hii tabia ya Yohoyakimu unapaswa kuiepuka katika maisha yako, kwa sababu kitakachokupata siku ile roho yako inatoka ndani ya huo mwili wako yatakuwa ni majuto ya milele (utakapokuwa unaenda JEHANAM ya moto), kwani Mungu Na Yeye atakudhihaki siku hiyo kama na wewe unavyodhihaki maonyo Yake leo hii.

Mithali 1:24 KWA KUWA NIMEITANANYI MKAKATAANIMEUNYOSHA MKONO WANGUASIANGALIE MTU

25 Bali mmebatilisha shauri langu, WALA HAMKUTAKA MAONYO YANGU

26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, NITADHIHAKI hofu yenu ifikapo; 

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA KWANZA).


KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA PILI).


Kwanini Gombo la chuo lililokunjuliwa mbele ya nabii Ezekiel likikuwa limejaa maombolezo, na vilio na Ole ndani yake? (Ezekieli 2:10).


KWANINI BIBLIA INAMFANANISHA IBILISI NA SIMBA ANGURUMAYE?


LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, AU ATAKAYENENA KATIKA JINA LA MIUNGU MINGINE, NABII YULE ATAKUFA.

LEAVE A COMMENT