Je! Ni kweli Ibrahimu na sara walikuwa ni ndugu wa baba mmoja? (Mwanzo 20:12), Na kama ni ndio, kwanini Mungu aliruhusu ndugu hao kuoana?

SWALI: Naomba majibu ya swali hili, Je! Ni kweli Ibrahimu na sara walikuwa ni ndugu wa baba mmoja kulingana na (Mwanzo 20:12)? Na kama ni ndio, kwanini Mungu aliruhusu Ibrahimu kumchukua ndugu yake kama mke?

Mwanzo 20:11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu. 

12 NAYE KWELI NI NDUGU YANGUBINTI WA BABA YANGU ILA SIYE MWANA WA MAMA YANGU, ndipo akawa mke wangu. 

JIBU: Jibu ni ndio, Ibrahimu na Sara walikuwa ni ndugu wa baba mmoja, yaani Sara alikuwa ni binti wa Tera baba yake Ibrahimu lakini kwa mama mwengine.

Mwanzo 20:12 Naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila siye mwana wa mama yangu, ndipo akawa mke wangu. 

Kwa sababu Tera alizaa wana wa kike na wa kiume pia ambao ni Abramu, Nahori na Harani, na mke wa Nahori alikuwa Milka mtoto wa Harani, hivyo ni ndugu kwa ndugu hao walioana.

Mwanzo 11:27 Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. 

28 Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. 

29 Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. 

Lakini si hao tu walioowana ndugu kwa ndugu, bali hata Isaka mwana wa Ibrahimu, alimuoa Rebeka ndugu yake mtoto wa Bethueli ambaye alikuwa ni mtoto wa Nahori ndugu yake Ibrahimu.

Mwanzo 22:20 Ikawa baada ya mambo hayo, Ibrahimu akaambiwa ya kwamba, Tazama, Milka naye amemzalia Nahori ndugu yako wana; 

21 Usi, mzaliwa wa kwanza wake, na Buzi nduguye, na Kemueli, baba wa Aramu; 

22 na Kesedi, na Hazo, na Pildashi, na Yidlafu, na BETHUELI

23 BETHUELI AKAMZAA REBEKA; hao wanane Milka alimzalia NAHORI NDUGU WA IBRAHIMU

Huyo Rebeka mwana wa Bethueli mwana wa Nahori ndugu yake Ibrahimu (Mwanzo 11:27), ndiye aliyekuja kuwa mke wa Isaka mwana wa Ibrahimu, hivyo ni ndugu kwa ndugu wanaoana.


Mwengine ni Yakobo mtoto wa Isaka, yeye alioa mabinti wa mjomba wake, yaani mabinti wa kaka wa mama yake aliyeitwa Labani.

Mwanzo 24:29 NA REBEKA ALIKUWA NA KAKAJINA LAKE LABANI. Labani akatoka mbio kumwendea yule mtu kisimani. 

Na mabinti wa Labani ndio waliokuja kuolewa na mtoto wa Rebeka dada yake, hao pia ni ndugu kwa ndugu kabisa.


Sasa je! Na sisi sasa hivi tunaruhusiwa kuoa mabinti za baba zetu, wajomba zetu na mashangazi zetu, au na mabinti za baba zetu wakubwa na wadogo? 

Jibu ni hapana, Mungu alisema hivi katika Mambo ya Walawi.

Walawi 18:6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana. 

Soma tena 

Walawi 18:9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.

Soma na tena. 

Walawi 18:11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. 

12 Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. 

Lakini ni kwanini sasa Mungu aliruhusu wakina Ibrahimu, Sara, Isaka, Rebeka, Nahori, Milka, Yakobo, Lea, Raheli, n.k kuoana ndugu kwa ndugu? Na tena mtu kama Ibrahimu alisisitiza mwanawe Isaka akatafutiwe mke kwa watu wa nyumba ya baba yake? na sio nje kama tulivyoona kwenye maandiko? 


Jibu ni kuwa, kitendo hicho kilikuwa ni ujumbe na ufunuo wa Mungu kwa kanisa lake ambalo pia ni ndugu wa Baba Mmoja KATIKA BWANA, kwa kubatizwa kwa jina Lake na kupokea Roho Wake kwamba, wanapaswa kuoana wao kwa wao (ndugu katika roho), na si vinginevyo, na ndio maana mtume Paulo alisema..

1 Wakorinto 9:5 Hatuna uwezo kuchukua PAMOJA NASI MKE ALIYE NDUGU, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa? 

Au soma tena

1 Wakorinto 7:39 Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; KATIKA BWANA TU

Huo ndio ufunuo wake hapo, hivyo kama wewe upo ndani ya mwili wa Kristo sawasawa na maandiko matakatifu, na bado hujaoa au kuolewa, basi tambua kwamba unapaswa kuoa au kuolewa na ndugu yako katika Bwana tu (rohoni), na sio ndugu yako wa kimwili (maandiko yamekataza).

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?


UMESHAIFAHAMU NA KUIPOKEA BARAKA YA IBRAHIMU KATIKA MAISHA YAKO .


MCHUNGAJI WAKO NI NANI?


Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema “Kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia” Je! Alikuwa akijigamba?(Wafilipi 3:6)


TABIA YA YEHOYAKIMU INAYOENDELEA SASA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO.

4 thoughts on - Je! Ni kweli Ibrahimu na sara walikuwa ni ndugu wa baba mmoja? (Mwanzo 20:12), Na kama ni ndio, kwanini Mungu aliruhusu ndugu hao kuoana?

LEAVE A COMMENT