MADHARA YA KULISIKIA NENO LA MUNGU NA KUTOWAZA  KUCHUKUA UAMUZI WO WOTE ULE WA KULIFANYIA KAZI (KULITII)

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Kuna madhara makubwa mno pale ambapo mtu anapolisikia neno la kweli la Mungu, na kisha kulipuuzia kwa makusudi  kabisa kwa kutokuwaza moyoni mwake na kuona ni namna gani afanye ili aweza kulitii neno hilo la Mungu, ama kwa kuchunguza kwanza ili kuona na kuthibitisha alichoambiwa, au kwenda mwenyewe binafsi kwa Muumba na kumuomba amsaidie kilithibitisha neno lake n.k, (mtu kama huyo anayelisikia na kulipuuzia neno la Mungu, maandiko yanasema adhabu yake itakuwa ni kubwa siku ya hukumu, maana ni afadhali asingelisikia kabisa neno hilo).


Sasa Ili kuelewa vizuri, hebu tusome vifungu vifuatavyo vya kwenye maandiko matakatifu (zingatia maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa).

Matayo 10:14 Na MTU asipowakaribisha WALA KUYASIKIA MANENO YENU, mtokapo katika NYUMBA ILEAU MJI ULE, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 

15 AMINNAWAAMBIAITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMUKULIKO MJI ULE

Soma tena

Luka 10:10 Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, 

11 Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. 

12 Nawaambia ya kwamba SIKU ILE ITAKUWA RAHISI ZAIDI SODOMA KUISTAHIMILI ADHABU YAKE KULIKO MJI HUO.

Ukisoma hapo kwa makini utagundua kuwa, Bwana ametoa sababu ya kwanini mji ule (watu wa huo mji), kustahiri adhabu kubwa kuliko miji ya sodoma na Gomora (watu wa sodoma na Gomora), katika siku ile, na sababu aliyoitoa Bwana hapo ni kuwa, WALISIKIA NENO LA MUNGU LAKINI WALIKATAA KUSIKILIZA (kulipokea mioyoni mwao na kulifanyia kazi ili walitii).


Jambo hili linaogopesha mno na kutisha sana, kwani kwa kadiri tunavyoisikia injili ya Kristo iliyohubiriwa na mitume wake na manabii wake (Maandiko matakatifu), na kuzidi kuikataa (kwa kupuuzia na kutokuwa na mpango wo wote ule), na ndivyo adhabu yetu siku ya Hukumu inatakavyokuwa kubwa. (Haijalishi wewe ni nani).


Ndugu mpendwa, ni mara ngapi unasoma maandiko na kuonywa juu uongo na utukanaji kwamba watu hao hawana sehemu katika ufalme wa Mungu lakini wewe unapuuzia na wala hauna mpango wote ule? 


Ni mara ngapi unaonywa juu ya rushwa na udhalimu unaoufanya? Ni mara ngapi unaonywa juu ya ushoga, usagaji, na ulawiti unaoufanya? Ni mara ngapi unaonywa juu ya mke wa mtu au mume wa unayeishi nae? Ni mara ngapi unaonywa juu ya binti au kijana unayeishi nae na huku hamjafunga ndoa kwamba watu kama hao hawana sehemu katika ufalme wa Mungu lakini wewe hutaki kusikia na wala huna mpango wo wote ule? 

1 Wakorinto 6:9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU?MSIDANGANYIKEWAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, WALA WAFIRAJIWALA WALAWITI

10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala WATUKANAJI, wala wanyang’anyi. 

Ni mara ngapi unaonywa na biblia juu ya umbea na usengenyaji? Ni mara ngapi unaonywa na maandiko juu chuki, vinyongo, na tabia yako ya kutokuwasamehe wengine kwamba usipowasamehe na wewe Mungu hatokusamehe lakini wewe hutaki kusikia na huna mpango wo wote ule?

Matayo 6:15 Bali MSIPOWASAMEHE WATU MAKOSA YAO, wala BABA YENU HATAWASAMEHE NINYI MAKOSA YENU

Ni mara ngapi unaonywa juu ya uchawi wako na uganga wako unaoufanya? Ni mara ngapi unaonywa juu ya kwenda kwa waganga lakini wewe hutaki kusikiliza na tena huna mpango wo wote ule?


Ni mara ngapi unaonywa na maandiko juu ya kuwaomba wafu kwamba ni machukizo kwa Mungu, na tena wachukizao wote sehemu yao ni katika ziwa la moto? (Ufunuo 21:8), Lakini wewe hutaki kusikia na wala huna mpango wo wote ule?

Kumbukumbu la Torati 18:10  Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE  WAFU

12 KWA  MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 

Ni mara ngapi unaonywa juu ya kutazama picha za ngono? Miziki ya kidunia iliyojaa maudhui ya uzinzi na uasherati, ni mara ngapi unaonywa juu ya filamu za kidunia zilizojaa maudhui ya ngono, matusi, uasherati n.k, kwamba ni najisi kwako, hivyo tofautisha kati ya vilivyo najisi na visivyo lakini wewe hutaki kusikia na huna mpango wo wote ule?

Walawi 10:10 kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyo najisi na hayo yaliyo safi; 

Ni mara ngapi unaonywa na kusikia juu ya uvaaji vimini na masuruali kwa Mwanamke ni dhambi na hutaki kusikia, na tena huna mpango wo wote ule? Ni mara ngapi unaonywa juu ya mapambo bandia kwa Mwanamke (mawigi, rasta, kucha bandia, hereni, mikufu, vikuku, n.k), na hutaki kusikia? 


Ni mara ngapi unaonywa juu ya kutubu dhambi zako, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na wa kimaandiko, na kupokea Roho Mtakatifu aliye muhuri wake Mungu lakini wewe hutaki kusikia na wala huna mpango wo wote ule Na kibaya zaidi unapinga?


Ndugu mpendwa, tambua kuwa, kwa kadiri unavyosikia maneno ya mitume (injili ya Kristo au maandiko matakatifu), na kuikataa kwa kutokuwa na mpango wo wote ule wa kuitii au kuutafuta ukweli wake, ndivyo adhabu yako inavyoongezeka na kuwa kubwa siku ile ya hukumu.

Matayo 10:14 Na MTU asipowakaribisha WALA KUYASIKIA MANENO YENU, mtokapo katika NYUMBA ILEAU MJI ULE, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 

15 AMINNAWAAMBIAITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMUKULIKO MJI ULE

Hivyo basi, itii injili ya Kristo (kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa kwa jina lake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako naw utapokea Roho wake), na wala usifanye moyo wako kuwa mgumu pindi usikiapo maneno ya maandiko kama wayahudi wa Korintho 

Matendo Ya Mitume 18:5 Hata Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. 

6 Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.


Mada zinginezo:

Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema “Kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia” Je! Alikuwa akijigamba?(Wafilipi 3:6)


TABIA YA YEHOYAKIMU INAYOENDELEA SASA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO.


Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?


Nini maana ya mstari huu “Nimesulubiwa pamoja na Kristo?” (Wagalatia 2:20)


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.

3 thoughts on - MADHARA YA KULISIKIA NENO LA MUNGU NA KUTOWAZA  KUCHUKUA UAMUZI WO WOTE ULE WA KULIFANYIA KAZI (KULITII)

  • amen, lakini bwana yesu alituachia maagizo mengi yakuashika, na tena bwana yesu ndiye aliyetuumba na madhaifu mbalimbali
    PALE MADHAIFU YETU YANAPOTUZUHIYA KUSHIKA MAAGIZO YA BWANA TUFANYE JE?

  • mfano kuimba, mimi ninarafiki yangu ajuwi kuimba kabisa kabisa, yaani akifumbua kinywa chake aimbe anahiya kuchekwa nahata kama uwe wewe ahupendi kucheka; utamcheka tu kwaginsi anavyoimba na jambo ilo imekuwa changamoto yake kubwa sana kwakuwa amehacha hadi ibada za asubui na hata za siku ya mungu kwasababu hiyo kwakuwa akikaa kimya kanisani wanamcheka, akiimba njo wanamcheka zaidi, sasa kama huyo afanye je?

LEAVE A COMMENT