IKAWA, MFALME ALIPOYASIKIA MANENO YA TORATI, ALIYARARUA MAVAZI YAKE.

Biblia kwa kina, Uncategorized 4 Comments

Siku moja mfalme Yosia katika wakati wa kutawala kwake, aliagiza ukarabati wa nyumba ya Bwana, kwa kuwatuma Shafani mwana wa Azalia, Maaseya Akida wa mji, na Yoa mwana wa Yoahazi, kwenda kwa Hilkia kuhani kwa lengo la kuihesabu fedha inayoletwa nyumbani mwa Bwana ili wapate kukarabati nyumba ya Bwana.

2 Wafalme 22:3 Ikawa, katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia, mfalme akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, mwandishi, nyumbani kwa Bwana, akisema, 

4 Enenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, ili aihesabu fedha yote inayoletwa nyumbani mwa Bwana, ambayo mabawabu wameipokea kwa watu; 

5 tena waitie ile fedha katika mikono ya wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya Bwana; wakapewe wafanya kazi waliomo ndani ya nyumba ya Bwana, ili wapate kupatengeneza mahali palipobomoka ndani ya nyumba; 

Soma tena 

2 Mambo ya Nyakati 34:8 Hata katika mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake, alipokwisha kuisafisha nchi, na nyumba, akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, na Maaseya, akida wa mji, na Yoa, mwana wa Yoahazi, mwandishi wa tarehe, waitengeneze nyumba ya Bwana, Mungu wake. 

9 Wakamjia Hilkia kuhani mkuu, wakampa fedha, iliyoletwa nyumbani mwa Mungu, waliyoikusanya Walawi, wangoje mlango, mikononi mwa Manase na Efraimu, na mabaki yote ya Israeli, na Yuda yote na Benyamini, na wenyeji wa Yerusalemu. 

(Sasa kwa undani wa habari za mfalme Yosia, unaweza soma kwa muda wako binafsi kitabu cha 2 Wafalme 22 au kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati 34).


Lakini kipindi ukarabati wa nyumba ya Bwana ulipokuwa ukiendelea, Hilkia Kuhani mkuu alikiona kitabu cha torati katika nyumba ya Bwana, (ambacho ndani yake mliandikwa maagizo ya Mungu na ghadhabu na laana pindi watakapoenda tofauti na yote yaliyoandikwa humo)

2 Wafalme 22: 8 Naye HILKIAKUHANI MKUUAKAWAAMBIA SHAFANIMWANDISHINIMEKIONA KITABU CHA TORATI KATIKA NYUMBA YA BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma. 

Na baada ya Shafani kukisoma kile kitabu, akaenda pia kukisoma mbele ya mfalme Yosia. Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maagizo yote ya torati na ghadhabu na laana zilizoandikwa mle, MFALME ALIYARARUA MAVAZI YAKE, kwa sababu ghadhabu na laana zote zilizoandikwa mule ndizo walizozistahiri kwa sababu baba zao hawakuyaangalia maneno ya kitabu kile na kufuata kama walivyoagizwa.

2 Mambo ya Nyakati 34:18 Shafani mwandishi akamweleza mfalme, akisema, HILKIA KUHANI AMENIPA KITABUSHAFANI AKASOMA NDANI YAKE MBELE YA MFALME

19 IKAWAMFALME ALIPOYASIKIA MANENO YA TORATIALIYARARUA MAVAZI YAKE

20 Mfalme akawaamuru Hilkia, na Ahikamu, mwana wa Shafani, na Abdoni, mwana wa Mika, na Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme, kusema, 

21 Nendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, katika habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya Bwana ni nyingi iliyomwagika juu yetu, KWA SABABU BABA ZETU HAWAKULISHIKA NENO LA BWANAKUTENDA SAWASAWA NA YOTE YALIYOANDIKWA KITABUNI HUMO

Hivyo ndivyo Yosia alivyofanya baada ya kusikia maneno ya torati na kujinyenyekeza mbele za Mungu kwa kurarua Mavazi yake baada ya kutambua makosa waliyomkosa Mungu na ghadhabu zitakazo wapata zilizo andikwa humo.

Lakini kama tunavyojua kwamba, mambo hayo yote yaliyokwisha kuandikwa, yaliandikwa kwa jinsi ya mifano ili kutufundisha na kutuonya sisi watu wa sasa. 

Warumi 15:4 Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. 

Hivyo basi, lipo funzo nyuma ya habari hiyo ambayo ni kuwa, hata sasa Torati ya Mungu, ambayo ni Injili ya Yesu Kristo iliyohubiriwa na mitume wake watakatifu bado ina maagizo yale yale, laana zile zile, na ghadhabu zile zile endapo wewe unayejiita mkristo ukienda tofauti na yale yaliyoagizwa katika Injili kwamba, utakumbana nazo tu kwani torati ndio Injili ya Kristo iliyohubiriwa na mitume wake, kwani mitume hawakuhubiri yaliyotofauti na hayo kama Paulo alivyosema katika

Matendo ya Mitume 26:22  Basi kwa kuwa nimeupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hata leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, WALA SISEMI NENO ILA YALE AMBAYO MANABII NA MUSA WALIYASEMA, kwamba yatakuwa;

Maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa, yale yote yaliyosemwa na Torati na manabii ndiyo hayo hayo yaliyohubiriwa na mitume (Injili ya Yesu Kristo), kwa ufunuo wa Roho wa Yesu Kristo Yule Yule aliyewaongoza manabii.

1 Petro 1:10 Katika habari ya wokovu huo MANABII walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, AMBAO WALITABIRI HABARI ZA NEEMA ITAKAYOWAFIKIA NINYI

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa NA ROHO WA KRISTO ALIYEKUWA NDANI YAO, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 

12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, AMBAYO SASA YAMEHUBIRIWA KWENU NA WALE WALIOWAHUBIRI NINYI INJILI KWA ROHO MTAKATIFU aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia. 

Hivyo, pindi usikiapo maneno ya Injili (Torati), kwamba Ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa mwili wako katika maji na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na kwamba, hakuna Mkristo yo yote yule kwenye maandiko aliyebatizwa vinginevyo, basi, unatakiwa kularurua moyo wako mbele za Mungu (na si Mavazi yako tena), maana baba zako hawakuzingatia yaliyoagizwa na injili kwa kukubatiza vingine kwani ghadhabu ya Mungu juu ya wote wasioamini na kubatizwa kama Yeye alivyoagiza ni kuu mno (Marko 16:16).


Unaposikia maneno ya kweli ya Injili, yaliyokinyume na dini yako au dhehebu lako, au yote uliyoyaamini na kufundishwa na baba zako, basi unapaswa kularurua moyo wako na kuanguka mbele za Mungu kwa kuomba rehema na msamaha kwa sababu dhehebu lako au baba zako hawakuzingatia na kuitii injili maana ghadhabu ya Mungu juu ya wote wasioitii Injili ya Yesu Kristo ni kuu mno (ni maangamizi ya milele na kutengwa na Utukufu wa nguvu zake).

2 Wathesalonike 1:8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, NA WAO WASIOITII INJILI YA BWANA WETU YESU

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?


TAFUTA SULUHISHO NA KULIFANYIA KAZI MAPEMA KABLA HUJAFIKWA NA UBAYA


TABIA YA YEHOYAKIMU INAYOENDELEA SASA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO.


YOSHUA MWANA WA NUNI.


YEROBOAMU MWANA WA NEBATI.


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)

4 thoughts on - IKAWA, MFALME ALIPOYASIKIA MANENO YA TORATI, ALIYARARUA MAVAZI YAKE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *