Moja ya tabia isoyopaswa kuwepo ndani yako katika siku hizi za mwisho ni na tabia ya kushindwa kutafuta suluhisho mapema kabla ubaya haujatufika. Leo kwa neema za Bwana, tutajifunza kutoka kwa Sedekia mfalme wa Yuda, ambaye alikuwa na tabia hiyo hiyo ya kushindwa kutafuta suluhisho na kulifanyia kazi mapema hadi mabaya yalipomkuta.
Sedekia mfalme wa Yuda aliletewa taarifa mbaya kutoka kwa Bwana kwa mkono wa Yeremia nabii kwamba, Mungu atautia mji wa Yuda katika mikono ya mfalme wa Babeli, na tena, yeye Sedekia mfalme atatiwa katika mikono ya Nebukadneza mfalme na kuchukuliwa utumwani mpaka Babeli. (Kwa urefu wa habari hiyo unaweza soma Yeremia 21: 1-8).
Lakini katika hali kama hiyo, uamuzi aliouchukua mfalme Sedekia ulikuwa ni wa tofauti kidogo, kwa sababu katika hali ya kawaida, mtu unapoletewa habari kama hii, kitu cha kwanza utakachokifanya ni kutafuta suluhisho mapema na kuuliza ni nini ufanye au ni kwa njia gani unaweza epukana na hatari hiyo. Ila kwa Sedekia yeye ilikuwa tofauti kidogo, yeye baada kutafuta Suluhisho mapema (na hata aliposhauriwa nini cha kufanya aliogopa kutii), yeye alichoamua kufanya ni kumtia gerezani kabisa nabii Yeremia, na kumwambia kwanini unasema maneno mabaya juu yangu na juu ya mji huu?
Yeremia 32:2 Basi, wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli liliuzunguka Yerusalemu; na Yeremia, nabii, alikuwa amefungwa ndani ya uwanda wa walinzi, uliokuwa katika nyumba ya mfalme wa Yuda.
3 KWA MAANA SEDEKIA, MFALME WA YUDA, ALIKUWA AMEMFUNGA, AKISEMA, KWA NINI UNATABIRI, NA KUSEMA, BWANA ASEMA HIVI, Angalia, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atautwaa;
4 TENA, SEDEKIA, MFALME WA YUDA, hatapona kutoka katika mikono ya Wakaldayo, lakini hakika yake atatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli, atanena naye mdomo kwa mdomo, na macho yake yatatazama macho yake;
5 naye atamchukua Sedekia mpaka Babeli, naye atakuwako huko hata nitakapomjilia, asema Bwana; mjapopigana na Wakaldayo hamtafanikiwa.
Uamuzi huo ulikuwa si wa hekima na wala si wa busara kabisa, kwa sababu, alipoletewa taarifa hiyo alipaswa kutafuta suluhisho mapema ili kuokoka na hiyo hatari. Lakini si hivyo tu, pia hata pale alipopewa ushauri wa nini cha kufanya aliogopa kufanyia kazi, na hatimaye maneno yote hayo ya Bwana yakatimia juu yake kama mjumbe wa Bwana alivyosema, watoto wake wa kiume walichinjwa mbele yake na yeye mwenyewe kupofushwa macho na kupelekwa Babeli utumwani.
Yeremia 52:10 Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake; pia akawaua wakuu wote wa Yuda huko Ribla.
11 Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake.
KUFUNUA NINI?
Kitu hichi hichi na tabia hii hii ndiyo inayoendelea sasa siku hizi za mwisho, leo hii Mungu bado anatoa taarifa mbaya kwa wanadamu wote chini ya jua kwa kutuambia Ghadhabu yake ipo tayari kwa wasio itii injili yake (Isaya 28:22), na endapo tutakaposhindwa kutafuta suluhisho mapema, basi, ubaya wote alioutamka Bwana utatimia juu yetu vile vile kama ulivyotimia juu ya Sedekia.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, unapopewa taarifa kwamba, waabudu Sanamu wote sehemu yao ni katika ziwa la moto, usisubiri mpaka iyo siku ikukute ndipo uamini, unapoambiwa ye yote ambaye jina lake halikuonekana katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo alitupwa katika ziwa la moto, usianze kusema, acha kuhukumu, bali tafuta suluhisho mapema la nini cha kufanya, ukiambiwa asiyemwamini Mwana hataona uzima bali ghadhabu ya Mungu inamkalia, usisubiri hadi hiyo siku ifike, tafuta suluhisho mapema, unapoambiwa wachukizao wote (mfano wanaume wanaovaa nguo ziwapasazo wanawake, na wanawake wanaovaa nguo viwapasazo wanaume), sehemu yao ni katika ziwa moto, usingoje mpaka hiyo siku ifike ndipo uamini, tafuta suluhisho sasa (mapema), kwani Bwana amenana ya yatakuwa tu, vinginevyo yatakukuta kama yaliyomkuta Sedekia.
Bwana akubariki, Shalom.
Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.
+255652274252/ +255789001312
Mada zinginezo:
NI BWANA GANI HUYO AMBAYE MANABII WALITABIRI KWA JINA LAKE NA KUTESWA KWA AJILI YAKE?
KWA SABABU NALIWAOGOPA WALE WATU, NIKATII SAUTI YAO.
FAHAMU NINI MAANA YA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24)
Kwanini Sanduku la Mungu lilitwaliwa na Wafilisti huko shilo? (1 Samweli 4:11)