JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?

Dhambi, Uncategorized 2 Comments

SWALI: Je! Ni dhambi mbele za Mungu kwa Mwanamke na mwanamume kuishi pamoja na kufanya tendo la ndoa pasipo kufunga ndoa kulingana na biblia?


JIBU: Ndio, mwanamume ye yote yule anayeishi na mwanamke na kufanya nae tendo la ndoa, na huku hawajafunga ndoa, wanafanya dhambi mbele za Mungu, haijalishi wanapendana kiasi gani, au wameishi hivyo kwa muda mrefu kiasi gani, au wamezaa watoto wengi kiasi gani, mahusiano kama hayo mbele za Mungu ni ya KIASHERATI, na tena usidanganyike, endapo ukifa katika hali hiyo pasipo kutubu na kurekebisha hicho kitu sasa wakati ukiwa hai, fahamu kuwa, hutokuwa na sehemu katika ufalme wa Mungu kwa sababu maandiko yapo wazi sana juu ya hilo.

1 Wakorinto 6:9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? MSIDANGANYIKEWAASHERATI HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 

Soma tena.

Waefeso 5:5 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 

Hivyo basi, kama wewe kijana wa kiume au wa kike, ulikuwa unaishi na huyo mwenzako kiholela holela tu, na kufanya nae tendo la ndoa kiholela holea, mnapaswa kutambua kuwa, ninyi ni waasherati mbele za Mungu, na mnafanya uasherati, mnachotakiwa kufanya ni kutubu na kuacha hicho kitu mara moja, na kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zenu (kama hamkufanya hivyo), na ndipo mfuate taratibu za kubaliki ndoa kanisani kama mlivyopanga.


Lakini wewe kijana wa kiume au wa kike, ambaye bado hujaingia katika mahusiano hayo ya kiasherati, unatakiwa kuwa hivyo hivyo mpaka utakapofunga ndoa, jiepushe na vishawishi na vichochezi vyote vya uasherati (zikimbie tamaa za ujanani ), kaa mbali na mrafiki na makundi mabaya, kaa mbali na kutazama picha za uchi katika mitandao na kwenye internet, na dumu katika utakatifu kwa kumcha Mungu

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

JE! KUJICHUBUA NI DHAMBI KULINGANA NA MAANDIKO?


Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?


Ufisadi ni nini katika maandiko?(Waefeso 5:18)


BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO 


KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)

2 thoughts on - JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?
  1. shalom!!! huku kwetu kunahali ya umaskini sana na kunawatu ambao awana uwezo wakufunga ndoa kwakisa cha umaskini wanaishia kufunga ndoa ya asili ambayo nikurendeza tu, je mungu atumbui ndoa hio? vio wakikutana kimwili ni uasherati mbele za mungu?

  2. Kama ni wakristo wanafanya uasherati, wanachotakiwa kufanya ni kwenda kanisani na kufungishwa ndoa (kuombewa mbele za Mungu kama wao ni mwili mmoja).

    Kumbuka: ndoa ni jambo la kuombewa kanisani tu, wala hakuna gharama yo yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *