Nini maana ya mstari huu “Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu” (Mithali 29:12)

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

JIBU: Tusome.

Mithali 29:12 Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu. 

Mstari huo unawahusu watu wote wanao tawala, au wenye dhamana ya kuongoza watu fulani au kundi fulani la watu, awe kiongozi wa kiserikali, kiongozi wa famalia au kiongozi wa kanisa. Yoyote yule katika hao, akisikiliza uongo na kuukubali na kuupokea, basi anawakosesha walio chini yake na kuwafanya kuwa na hati kwa sababu uongo siku zote upo kinyume na neno la Mungu na kamwe hauwezi urithi uzima wa milele.

Uongo huo unatoka wapi? 

Uongo huo ni kutoka kwa ibilisi, kwa sababu maandiko yanasema Yeye ndiye baba wa huo (Yohana 8:44).

Sasa zifuatazo ni baadhi ya sehemu tu, ambazo watu wenyewe kuongoza wakisikiliza uongo, basi wanawakosesha wale wanaowaongoza na kuwafanya kuwa waovu.


KATIKA FAMILIA.

Mfano wa hawa ni famalia za taifa la Yuda, ambao walisikiliza uongo wa kuabudu miungu mengine na kuwafanya watoto wao kuwa waovu na kuangamia kwa upanga, njaa, na tauni.

Wewe kiongozi katika familia (baba), au mama (kwa wale waliofiwa na baba), endapo ukisikiliza uongo na kuuamini huo, basi fahamu kuwa, anawafanya watoto wako kuwa waovu na wakosefu mbele za Mungu.

Kwa Mfano; Baba au mama, unaposikiliza uongo kwamba, kuvaa suruali kwa binti yako haina shida, basi tambua kuwa unamfanya huyo binti yako kuwa muovu na ACHUKIZAYE mbele za Mungu, kwa sababu biblia inasema mwanamke anayevaa mavazi yampasayo mwanamume ni machukizo kwa Bwana.

Kumbukumbu La Torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi YAMPASAYO mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO. 

Unaposikiliza uongo na kuwafundisha watoto wako kuwaomba wafu kama vile wakina Yosefu, Yasinta, Paulo, Emakulata n.k, fahamu kuwa, unawafanya watoto wako kuwa waovu kwa sababu kila ANAYE WAOMBA WAFU ANAFANYA MACHUKIZO.

Kumbukumbu La Torati 18:10  Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE  WAFU.

12 KWA  MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 


KATIKA SERIKALI.

Mfano wa hawa ni mfalme wa Israeli, Yeroboamu Mwana wa Nebati, ambaye maandiko yanasema aliwakosesha Israeli (1 Wafalme 22:52) aliokuwa anawatawala kutokana na kusikiliza uongo wa mawazo yake kutoka kwa ibilisi.

Kiongozi, Unaposikiliza uongo wa ibilisi kwamba, ndoa za jinsia moja hazina shida, na kisha ukaruhusu hilo, basi tambua kuwa, wote watakaofanya hicho kitu kwa ruhusa yako, na wale wote wanaokusikiliza ambao hawana kweli ya Mungu ndani yao, unawafanya kuwa watenda dhambi, ni kama tu alivyofanya Mfalme Yeroboamu. (Na utatolea hesabu ya hicho kitu siku ya hukumu mbele za Mungu). 


KATIKA KANISA.

Kama wewe ni kiongozi wa kanisa, (Mchungaji, askofu, mwalimu n.k), unaposikiliza uongo wa ibilisi kwamba, Mungu hatazami mwili bali roho tu, mapambo hayana shida, kuuza pombe na sigara sawa tu, wewe si hautumii, ubatizo sio jambo la lazima sana na huku maandiko yanasema Aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini atahukumiwa, tambua kuwa unawafanya washirika wako kuwa waovu kwa kushindwa kumtii Mungu (utatolea hesabu siku ya mwisho).

Hivyo basi, kama bado unasikiliza uongo wa kiongozi wako (awe baba yako, mama yako, boss wako, au mchungaji wako), tambua kwamba unakoseshwa na kufanywa kuwa muovu, unachotakiwa kufanya ni kuukataa na kumweleza ukweli, ili wote muishi katika kweli kwa ajili ya usalama wa roho zenu, na kama bado hujampokea Kristo fanya hivyo sasa kwa kutubu dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha kabisa, na kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo ka dhambi zako.

Luka 6:39 Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili?

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Nini maana ya mstari huu “Hatukuja na kitu duniani, na tena hatuwezi kutoka na kitu? (1 Timotheo 6:7)


Ni mambo ya nyumba ipi ambayo mfalme Hezekia aliambiwa kuyatengeneza? (Isaya 38:1)


Nini maana ya mstari huu “unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu” (2 Petro 2:21) 


MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *