Je! Mitume wa Bwana walibatizwa?

Maswali ya Biblia, Uncategorized 2 Comments

SWALI: Naomba kuuliza, hivi katika maandiko mitume wa Bwana Wetu Yesu Kristo walibatizwa kweli?


JIBU: Ndio, mitume wa kweli wa Bwana Wetu Yesu Kristo walibatizwa katika maandiko, kwa sababu, ikiwa Yeye Mwenyewe Mwana wa Adamu alibatizwa (Mathayo 3:16), Ambaye ni Mtume Mkuu na wa kwanza, itakuwaje hao wengine.

Waebrania 3:1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana MTUME NA KUHANI MKUU wa maungamo yetu, YESU


Sasa hebu tutazame kwenye maandiko jinsi mitume wa Bwana walivyobatizwa.


MTUME ANDREA.

Huyu ni mmoja wa wale mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo, ambaye pia alikuwa ni ndugu yake na Mtume Petro.

Matayo 10:2 Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, NA ANDREA nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 

Andrea kabla ya kufanywa mtume na Bwana, alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana mbatizaji, ambaye alipokuwa na wanafunzi wake wawili (na Andraa akiwa ni mmoja wapo), walimsikia Yohana akisema, tazama Mwana Kondoo wa Mungu.

Yohana 1:40 ANDREANDUGUYE SIMONI PETROALIKUWA MMOJA WA WALE WAWILI WALIOMSIKIA YOHANA NA KUMFUATA YESU

Hivyo, kama Andrea alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji, basi ni wazi Kuwa alibatizwa kwa ubatizo wa Yohana kwanza, na kubatizwa tena kwa jina la Yesu Kristo kama wanafunzi wengine wa Yohana Mbatizaji walivyobatizwa (Matendo 19:4-5).


MTUME MATHIYA.

Huyo ni yule mwanafunzi aliyechukua nafasi ya mtume Yuda kwa kupigiwa kura, na baada ya kura kumwangukia, alihesabiwa kuwa mtume na wale kumi na mmoja hivyo kukamilisha idadi ya mitume 12.

Matendo 1:26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja. 

Mtume huyo Mathiya kabla, alikuwa ni mwanafunzi wa Yesu Kristo (hivyo alibatizwa), ambaye alifuatana na Bwana wakati wale 12 walipokuwepo, tangu mwanzo hadi kupaa kwake.

Matendo 1:21 Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, 

22 kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi. 


MTUME YAKOBO.

Mtume Yakobo huyu ni tofauti na mtume Yakobo mwana wa Zebebadayo ambaye ni ndugu yake na mtume Yohana 

Marko 3:17 na YAKOBOMWANA WA  ZEBEDAYONA YOHANA NDUGUYE YAKOBO, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; 

Yakobo mtume mwana wa Zebedayo aliuwawa mapema sana kwa upanga na mfalme Herode (Soma Matendo 12:2), lakini mtume Yakobo huyu ni mtoto wa Mariamu (Mathayo 13:55), ndugu wa tumbo moja na Bwana.

Wagalatia 1:19 LAKINI SIKUMWONA MTUME MWINGINEILA YAKOBONDUGU YAKE BWANA

Yakobo huyo alibatizwa yeye na ndugu zake kama wanafunzi wengine tu ambao waliomfuata Kristo, na hawa wote walikuwa pamoja (wakati wale kumi na moja wakiwepo kabla Mathiya kujaza nafasi ya Yuda). Kwa sababu ni lazima ubatizwe ili uwe mwanafunzi wa Yesu Kristo.


MITUME BARNABA NA PAULO.

Matendo 14:14 WALAKINI MITUME BARNABA NA PAULO, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, 

Mtume Barnaba

Huyu alikuwa ni mmoja wa jamaa wale walioamini na KUBATIZWA katika kanisa la pale Yerusalemu, Mlawi, mtu wa Kipro, Yusufu, ambaye aliitwa na mitume Barnaba.

Matendo 4:36 Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, 

37 alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. 

Hivyo, Barnaba kabla ya kuwa mtume, alikuwa ni mwanafunzi wa Bwana aliyebatizwa (kama wanafunzi wengine), na maandiko yanasema alikuwa ni mtu mwema, aliyejaa Roho Mtakatifu na imani (Matendo 11:24).


Mtume Paulo.

Mtume Paulo kama wengine, yeye alibatizwa na mwanafunzi wa Bwana aliyeitwa Anania baada ya kumwamini Yesu Kristo. Unaweza soma (Matendo ya Mitume 22:16) na (Matendo ya Mitume 9:17-18), utathibitisha hilo.

Na tena mtume Paulo alisema.

2 Wakorinto 11: 5 Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu. 

Kumaanisha kwamba, kama wao waliona maono, basi hata yeye pia, kama Wao walifufua wafu, basi hata yeye pia, kama wao, walitoa mapepo na kuponya viwete, basi hata na yeye pia, na kama wao walibatizwa, basi hata na Yeye pia.

Hivyo basi, kwa kuhitimisha ni kwamba, Mitume wa Bwana nao walibatizwa, na hata mitume wa sasa pia wa Bwana nao wanabatizwa, kwa ufupi kila atakaye mwamini Yesu Kristo ni lazima abatizwe kwa jina lake (hilo ni agizo la lazima kwa kila atakaye mwanimi Mwana wa Adamu, na si ombi).

Matendo 10:48 AKAAMURU WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Bwana Yesu alikuwa ni mdhambi kulingana na Mathayo 3:6? 

Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)


NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.


Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)


Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?

2 thoughts on - Je! Mitume wa Bwana walibatizwa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *