“NA VITABU VIKAFUNGULIWA” NI VITABU GANI HIVYO? (Ufunuo 20:12).

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

SWALI: Mtume Yohana kwenye maono yake, aliwaona wafu wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya kiti cha enzi (mbele za Mungu), kisha na VITABU VIKAFUNGULIWA. Swali ni je! Hivyo vitabu ni vipi au ni nini?

Ufunuo 20:12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; NA VITABU VIKAFUNGULIWA; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 

JIBU: Vitabu hivyo ni kumbukumbu ya matendo ya kila mwanadamu aliyoyafanya hapa duniani tangu ile siku yake ya kwanza, hadi siku yake ya mwisho, vitabu hivyo (kila mtu cha kwake), vitafunguliwa siku ile, na mwanadamu huyo (bila kujali yeye ni nani au alikuwa nani), atahukumiwa sawasawa na yale yaliyomo katika kitabu cha uzima, yaani neno la Mungu, au injili ya Kristo, iliyohubiriwa na Mitume na manabii wake watakatifu.

Warumi 2:16 KATIKA SIKU ILE MUNGU ATAKAPOZIHUKUMU SIRI ZA WANADAMUSAWASAWA NA INJILI YANGU, KWA KRISTO YESU

Kila jambo analolifanya mwanadamu duniani linarekodiwa katika kitabu chake (faili lake), na atakuja kutolea hesabu ya yote hayo siku ile mbele za Mungu (Yesu Kristo), yawe ni mema au mabaya.

Warumi 14:10 Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? KWA MAANA SISI SOTE TUTASIMAMA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA MUNGU

Soma tena.

2 Wakorinto 5:10 KWA MAANA IMETUPASA SISI SOTE KUDHIHIRISHWA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. 

Na Ikiwa rekodi za matendo ya mwanadamu huyo yatakuwa kinyume na neno la Mungu, basi, atatupwa katika ziwa la moto (ufunuo 20:15).


Wewe mvulana, ile siku ulipofanya uasherati na yule binti, tambua kuwa hicho kitu kilirekodiwa katika kitabu chako (faili lako). Wewe msichana, ile siku ulipo fanya uasherati yule mvulana, fahamu kuwa hicho kitu kilirekodiwa katika kitabu chako, ile siku uliyolala na mume wa mtu, ile siku uliyolala na mke wa mtu, ile siku uliyokula rushwa, ile siku ulipotukana, ile siku ulipo sema uongo, ile siku iliyofanya masturbation (punyeto), na kutazama picha za ngono, ile siku uliyoiba, ile siku uliyovuta sigara na kunywa pombe, ile siku ulipomtukana na kumpiga mama yako, ile siku uliyowaonea wanyonge, ile siku ulipofanya mauaji na ubakaji, ile siku uliyoenda kwa mganga, ile siku ulipoabudu sanamu na kuwaomba wafu, ile siku ulipovaa suruali na mavazi ya kikahaba mwanamke, ile siku uliyotoa mimba wewe binti, ile siku uliyoshiriki kwenye utoaji mimba daktari au nesi, ile siku uliyompiga mke wako, ile siku uliyoenda kulewa na kukesha night clubs, fahamu kwamba, hayo yote yalirekodiwa katika kitabu chako au faili lako, na tena, endapo yakibaki vivyo hivyo hadi siku ya kufa kwako pasipo kufutwa, utatupwa katika ziwa la moto.


Hivyo basi, fanya haraka sasa kuyafuta hayo katika faili lako, na njia pekee ya kuyafuta hayo sio kutoa hongo kama ulivyozoea kufanya hivyo katika faili la hapo Kazini kwako, hapana! Bali ni kwa damu ya Yesu Kristo, kwa njia ya kutubu dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha kabisa na kwenda kubatizwa kwa jina lake, ndipo hayo yatakapofutwa kwa kupata msamaha wa dhambi zako.

Matendo 2:38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTOMPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI.


Nini maana ya mstari huu “Hatukuja na kitu duniani, na tena hatuwezi kutoka na kitu? (1 Timotheo 6:7)


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


FAHAMU NINI MAANA YA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 08)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *