MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 08)

  Siku za Mwisho, Uncategorized

Jina kuu la Bwana Wetu na Mungu Wetu Yesu Kristo litukuzwe, nakukaribisha tena kwa mara nyingine katika mfululizo wa makala hii fupi inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayopotosha watu wengi nyakati hizi za mwisho, tulishayatazama baadhi ya hayo makanisa na mafundisho yao potofu huko nyuma katika sehemu zilizopita, (kama ulipitwa na sehemu hizo unaweza tutumia ujumbe kwa namba zilizopo mwishoni mwa somo hili). 

Hivyo, ukiona mahali ulipo katika kanisa lako ni moja wapo ya hayo na tayari umeshaufahamu ukweli, unachopaswa kufanya ni kuchukua hiyo biblia yako mkononi mwako, na kumfuata huyo kiongozi wako (awe Mchungaji, askofu, nabii, mtume, mwalimu, vyo vyote vile). 

Muulize ni wapi imeandikwa Mbinguni kuna viti vya enzi vitatu? Ni wapi ilipoandikwa Mariamu ni kimbilio la wakosefu? Ni wapi Mungu amekutuma wewe unifundishe mimi jinsi ya kupata majumba na magari badala ya kunifundisha utakatifu na kuacha dhambi? 

Mwambie akuoneshe ni mkristo gani katika maandiko (hata mmoja tu), aliyebatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho? Akishindwa mwambie kuwa, Wakristo wote kwenye maandiko walibatizwa kwa JINA LA YESU KRISTO, kwani hilo ndilo jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (mpe na maandiko), na kama yeye kweli ni wa Mungu, basi atatafakari na kujirekebisha na kusikia yaliyo ya Mungu maana imeandikwa, walio wa Mungu huyasikia yaliyo ya Mungu (Yohana 8:47), kama hataki MWACHE, maana ndivyo Bwana alivyosema, kwani huyo ni kipofu na kiongozi wa vipofu.

Matayo 15:14 WAACHENI; HAO NI VIONGOZI VIPOFU WA VIPOFU. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili. 


Na hii ni sehemu ya nane (08) ya makala yetu, karibu.


KANISA LINALOPINGA AGIZO LA  WANAWAKE KUFUNIKA VICHWA WAKATI WA IBADA.


Kanisa lolote lile lililo kinyume na agizo hilo la wanawake kufunika vichwa wakati wa ibada si la Mungu, halijarishi lina nini hapo. Viongozi wengi kwa kukosa uelewa wa maandiko, wanajikuta wakipinga agizo hilo kwa kisingizio kuwa, mwanamke amepewa nywele ndefu ili ziwe badala ya vazi (1 Wakorinto 11:15), hivyo hakuna haja ya kufunikwa kichwa, ndugu uo ni uongo wa ibilisi. Hebu jiulize, kama Paulo alisema zile nywele ni badala ya vazi na hakuna haja ya kufunikwa kichwa, sasa kulikuwa na haja gani tena ya kusema, Mwanamke ASIPOFUNIKWA NA AKATWE NYWELE? 

1 Wakorinto 11:6 Maana MWANAMKE ASIPOFUNIKWA NA AKATWE NYWELE. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe. 

Unaona hapo? Ikiwa na maana kuwa, maandiko yanamtaka mwanamke afunikwe kichwa chake zikiwemo na hizo nywele kichwani ndio maana kasema asipofunikwa na akatwe nywele (kuashiria nywele zinapaswa kufunikwa).

Hivyo basi, ukiona upo chini ya kanisa kama hilo linalopinga agizo la moja kwa moja kabisa, fahamu kuwa haupo sehemu sahihi, unachotakiwa kufanya ni kupaki vilago vyako na kutoka hapo (haijalishi Kanisa lako ni zuri kiasi gani). Lakini kama ukitaka kuleta fitina kuhusu Jambo hilo tambua kuwa, Makanisa ya Mungu hayana desturi kama hiyo.

1 Wakorinto 11:13 JE! INAPENDEZA MWANAMKE AMWOMBE MUNGU ASIPOFUNIKWA KICHWA?

14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?

15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.

16 LAKINI MTU YE YOTE AKITAKA KULETA FITINA, SISI HATUNA DESTURI KAMA HIYO, WALA MAKANISA YA MUNGU

Kumbuka: Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE.


LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.


KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.


AGIZO LA MUNGU KWA WATU WOTE.

LEAVE A COMMENT