VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE.

Mwanamke, Uncategorized 1 Comment

FUNDISHO MAALUMU KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.

Jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe, sifa na Utukufu ni vyake milele na milele, Amina. Karibu katika makala ya mafundisho maalumu kwa mwanamke wa kikristo. 


Moja ya vitu ambavyo maandiko yanawaagiza Wanawake wa kikristo wanaoukiri uchaji wa Mungu ni kujipamba kwa mavazi ya kujisitiri, yaani kutokuvaa mitaani nguo zinazoonesha sehemu za ndani za miliili yao na kuchora maungo yao mfano; kaptura, vimini, suruali n.k. Sambamba na hilo pia, wanatakiwa kuwa adabu nzuri, na moyo wa kiasi. Lakini pia maandiko hayaishii hapo tu, bali yanaenda mbele zaidi na kusema SI KWA KUSUKA NYWELE.

1 Timotheo 2: 9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; SI KWA KUSUKA NYWELE, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 

Wanawake wengi wa kikristo sasa hivi agizo hili la kutokusuka nywele zao za asili hawalifahamu, wengi wanadhani si sawa pekee kuweka wingi kichwani, au kupaka super black na kubadili rangi ya nywele, au si sawa pekee kusuka rasta tu na mapambo mengine mengine. Hayo ni sawa na si sahihi kabisa kwa mwanamke wa kikristo kuweka hivyo vitu, lakini biblia haijaishia hapo, imesisitiza pia suala la KUTOKUSUKA NYWELE kwa mwanamke anayeukiri uchaji wa Mungu (na ni katika agano jipya).

1 Timotheo 2: 9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; SI KWA KUSUKA NYWELE, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 

Soma tena

1 Petro 3:3 Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI, KUSUKA NYWELE; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 

Jambo hili linaweza kuwa jipya kwako na gumu kidogo kuingia alikini, lakini ukweli ndivyo ulivyo, siku zote tunapoitambua kweli ya maandiko matakatifu na kuifahamu, hatuna budi kuipokea na kuitii kwa kukubali kubadilika, kwa sababu maandiko matakatifu kazi yake ni kuturekebisha makosa yetu, kutuonya na kutuongoza katika kweli ili tupate kuwa kamili katika imani.

2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 

17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 

Lakini sasa unaweza jiuliza, nitafanyaje wakati mimi nywele zangu ni za kiafrika na sio kama za mzungu au mwarabu? 


Kwanza kabisa, unachopaswa kutambua ni hiki, agizo hilo la wanawake kutokosuka nywele, haliwahusu wanawake wa kiarabu peke yao au wanawake wa kizungu peke yao, la hasha! Bali ni agizo linalowahusu wanawake wote duniani wanaoukiri uchaji wa Mungu ukiwemo na wewe (1Timotheo 2:10). Na tena Mungu hakukosea na wala hakufanya makosa kukuumba wewe hivyo ulivyo na nywele zako, Yeye kwa hekima Yake kabla hujazaliwa, alishatambua na alishapanga namna gani ya kuzikuza nywele zako hadi utakapokufa (kwa sababu wewe hukujiumba mwenyewe), na ndio maana Akasema.

Matayo 5:36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana HUWEZI KUFANYA UNYWELE MMOJA KUWA MWEUPE AU MWEUSI

Kumaanisha kuwa, Yeye ndiye anyeshuhurika na hicho kichwa chako zikiwemo na hizo nywele zako, kuzibadili na kuzikuza katika hatua mbali mbali za ukuaji kwenye maisha yako, kutoka kuwa za kijana na kuzifnya kuwa mvi uzeeni. Hivyo basi, unachopaswa kufanya ni kumtii Yeye na hilo agizo lake kuhusu nywele zako, na kama ulikuwa umezisuka nenda kazifumue, zioshe kwa maji safi na sabuni, zikaushe vizuri kwa taulo, zipake mafuta ili ziwe laini na nzuri, zichane vizuri kwa chanuo au kitana, kisha uziweke na uzitunze katika asili yake. (Kuzikuza ni jukumu la Mungu).


Tafadhari washirikishe na wanawake wengine wa kikristo ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

MAMA MKWE WA KIKRISTO, JIFUNZE KITU KUTOKA KWA NAOMI.


FUNZO KATIKA HABARI YA MFALME AHABU NA NABII MIKAYA


KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)


Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?


Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)

One Reply to “VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *