JE! KUJICHUBUA NI DHAMBI KULINGANA NA MAANDIKO?

Dhambi, Uncategorized No Comments

JIBU: Ndio, kijichubua ni dhambi kulingana na maandiko, mwanadamu yo yote yule anayetumia madawa yo yote au kitu chochote kile kwa ajili ya kutaka kubadili rangi ya ngozi yake ambayo Mungu alimuumba anatenda dhambi, na pia anashindana na Muumba Wake, kwa sababu biblia inasema, Mungu alipofanya uumbaji wake hakukosea na wala hakukuwa na kasoro yoyote ile, na tena aliona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema.

Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, NA TAZAMANI CHEMA SANA. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita. 

Hivyo, unapojaribu kujichubua ngozi yako wewe mwanamke au wewe mwanamume,  ambayo Mungu amekuumba katika ukamilifu wote maana yake unashindana na Muumba Wako, unamwambia Mungu Umekosea kuniumba na rangi hii, Ulipaswa kinipa rangi ile, OLE WAKO wewe unayeshindana na Muumba wako, ndivyo maandiko yanavyosema.

Isaya 45:9 Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono? 

Hivyo, Mungu hakukosea katika uumbaji Wake na wala hakufanya mapungufu, kaa katika hali yako ya asili na umshukuru kwani umeubwa kwa jinsi ya ajabau 

Zaburi 139:14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,

Kama ulikuwa Ukifanya hivyo tambua kwamba ulikuwa ukifanya makosa, unachopaswa kufanya sasa ni kwenda mbele za Mungu kutubia kitu hicho na kuacha kabisa. 

Yeremia 13:23 Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya. 

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

Je! Ni dhambi kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali?


JE! MAPAMBO YA VITO NI DHAMBI?


Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?


Je! matumizi ya mimea ya asili kwa matibabu ni dhambi kwa mkristo?


Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *