Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?

SWALI: je! Ni sahihi kwa mtu aliyeokoka kufanya biashara ya uuzaji wa cheni (mikufu) na hereni?

JIBU: Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lipewe sifa milele na milele, inabidi ifahamike kuwa, si uuzaji wa cheni na hereni tu, bali hata uuzaji wa vipodozi, mawingi, kucha bandia n.k si sawa. 

Kwanini si sawa? Si sawa kwasbabu utumiaji wa hivyo vitu kwa mkristo ni dhambi na maandiko yamekataza, sasa kama wewe unafahamu kuwa utumiaji wa hivyo vitu si sawa na maandiko yanakataza, kwanini basi kwenda kuwauzia wengine? Unawahubiri watu kuwa kuvaa hereni si sawa, kujichubua si sawa lakini wewe mwenyewe ndiye unayewauzia, huoni kama unafanya dhambi? Maandiko yanasema hivi katika.

Warumi 2:21  basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe?

 22 Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu? 

Umeona hapo? unawahubiri wengine wasizini ila wewe unazini, unawahubiri wengine wasiibe ila wewe unaiba, unawahubiri wengine kuwa,uvaaji wa hereni na mikufu ni dhambi ila wewe ndo unayewauzia, unawahubiri wengine kuwa, kujichubua ni dhambi lakini wewe ndo unauza hivyo vipodozi, unawahubiri wengine kuwa ubandikaji wa kucha bandia na nyusi ni dhambi ila wewe ndo unayewauzia, utakua unafanya kitu gani sasa hapo?

Hivyo basi, kwa kuhitimisha ni kuwa, uuzaji wa hivyo vitu si sawa kwa mkristo, badale yake tunapaswa tuwe mstari wa mbele kwa kumea hivyo vitu na kuwaambia watu  watubu na kumwamini Kristo na kubatizwa na kuishi maisha ya utakatifu wa ndani na nje.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

MADA ZINGINEZO

JE! MAPAMBO YA VITO NI DHAMBI?


Je! Binti kujipamba mwili wake si ni jambo jema kwani atakua analipamba hekalu la Mungu?


Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?

2 thoughts on - Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *