AGIZO LA MUNGU KWA WATU WOTE.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Kwa zaidi ya mwaka sasa ni mvutaji wa sigara, kwa takriani miezi sita unafanya uasherati na uzinzi, unadanganya, unaabudu sanamu, unaenda kwa waganga, wewe ni askofu, mchungaji au nabii lakini unadanganya watu, unaishi na mke wa mtu, ni mlevi, unatembea nusu uchi na kuvaa suruali mwanamke, na kibaya zaidi yule mwanamke anayevaa mavazi ya kujisitiri una mcheka na kumdhihaki, unamwona kama ni mshamba kapitwa na wakati,


Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa bado ni mwizi na muuaji, bado ni mtukanaji kijana, mtu wa night clubs, mpenda anasa na starehe, kwa zaidi ya miaka sasa umemsaliti mke wa ujana wako kwa sababu ni mgonjwa, unaishi na mwanamke mwengine (unamkasilisha Mungu), umewatelekeza watoto wako, kwa zaidi ya wiki mbili sasa unachuki na kinyongo na jirani yako, ni mkaidi, unawatukana na kuwapiga wazazi wako, unavumisha habari za uongo na umbea, kwa miaka saba sasa ni mla rushwa na dhalimu, unawakandamiza wanyonge mayatima na wajane.


Japokuwa unayafanya yote hayo, lakini Mungu bado amekupa uhai na pumzi, umeamka na bado unahema, je! unadhani ni kwa sababu wewe ni hodari sana, au unadhani ni kwa sababu wewe ni mzuri sana, Je! unadhani ni kwa sababu una cheo fulani au una elimu fulani? Unadhani ni kwa sababu wewe ni kijana huwezi kufa? Unadhani ni kwa sababu wewe ni maskini sana au wewe ni tajiri sana? Jibu ni hapana, hizo ni huruma za Mungu tu! kwani hapendi ufe katika hali hiyo na kwenda kuzimu.

Maombolezo 3:22 Ni HURUMA ZA BWANA  KWAMBA HATUANGAMII, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.

23 Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. 

Mungu ametoa agizo lake kwa watu wote china ya jua ukiwemo na wewe unayeishi maisha hayo kwa muda mrefu sasa, lakini bado umepewa neema ya kuiona siku hii ya leo, kwamba UTUBU, bila kujali wewe ni nani, Mungu anakugiza UTUBU

Matendo 17:30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; BALI SASA ANAWAAGIZA WATU WOTE KILA MAHALI WATUBU.

Tubu kwa kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi, ambao ni wa kuzamishwa na kwa JINA LA YESU KRISTO, nawe utapata msamaha wa dhambi zako zote kabisa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, ambaye atakuwezesha kuishi maisha matakatifu na kukufundisha mapenzi ya Mungu na kuyafanya.

Matendo Ya Mitume 2:37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni MKABATIZWE KILA MMOJA WENU KWA JINA LAKE YESU KRISTO,mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Bwana akubariki. 

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Ni hukumu ipi ya Ibilisi inayozungumziwa katika Waraka wa (1 Timotheo 3:6?)


Ni maneno yapi ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo? (Kulingana na 1 Timotheo 1:18)


Msaidizi wa kufanana naye ni nani ambaye Mungu alimfanyia Adamu? (Mwanzo 2:18)


Ni Mungu gani tutakayemwona na kufanana nae atakapodhihirishwa? (1 Yohana 3:2)


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA APOLO.

LEAVE A COMMENT