Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?

SWALI: Je! Ni kweli kuwa, karama ya kunena kwa lugha haikupewa kipaumbele  katika kanisa na mtume Paulo kama makanisa mengi yanavyofanya leo hii?


JIBU: Makanisa mengi leo hii yanazimisha karama za Roho Mtakatifu kwa kutokuelewa maandiko, wengi wanahitimisha kwa kusema kuwa, alichokifanya Mtume Paulo ndicho tunachokifanya na sisi, mtume Paulo hakuipa kipaumbele karama ya kunena kwa lugha kutokana na vurugu zilizokuwa zikiendelea huko Korintho, hivyo kupelekea baadhi ya makanisa kupinga utendaji kazi wa karama hiyo ya kunena kwa lugha katika makanisa, lakini si karama hiyo tu, bali  hata na karama zingine nyingi kama uponyaji, miujiza, unabii, n.k  kwa kisingizio kuwa kumekuwa na machafuko mengi sana na upotoshaji mkubwa sana juu ya hizi karama za Roho.


Ni kweli kabisa kuwa, sasa hivi kumezuka wimbi kubwa mno la upotoshaji wa karama hizi kwa maslai binafsi, wengi wanapotosha watu kwa matumizi ya hizi karama, ama kwa kuwa nazo ama kwa kuongopa, lakini je! Na sisi tuzikatae na kuzipinga na kutokuzipa kipaumbele kwa sababu hiyo? Hasha! Kwani tukisema tuzikatae na kuzipinga karama hizi kutokana na upotoshwaji mkubwa sana unaofanywa na watu kwa maslahi yao binafsi, basi, hatuna budi pia KUIKATAA, NA  KUIPINGA, NA KUTOKUIPA KIPAUMBELE INJILI YENYEWE KABISA, kwani hata sasa pia kuna wimbi kubwa mno la upotoshwaji wa injili ya msalaba. Umeona? Je! Na sisi tupinge injili, na kutokuipa kimbaumbele kutokana na kuongezeka kwa wimbi kubwa la upotoshaji wa injili ya wokovu? Jibu ni hapana! Hivyo basi, hatupaswi kupinga karama la Roho Mtakatifu au injili ya Kristo kwa sababu tu! Kuna  vurugu na wimbi kubwa la upotoshwaji ulioenea sasa duniani, bali tunachotakiwa kufanya ni kuhubiri kwa kasi sana injili ya kweli wokovu na si kupinga wala kutoipa kipaumbele, kufundisha kwa kasi sana kuwa karama za Roho Mtakatifu ikiwemo ya kunena kwa lugha haifundishwi na mtu wala kujifunza sehemu yoyote ile isipokuwa Roho Mtakatifu anamjalia mtu kama apendavyo, tena tufundishe pia kwa kasi karama za kweli za Mungu na vigezo vyake, ili watu waweze kubaini mafundisho ya waalimu na manabii wa uongo yanayopotosha watu, na wala si kuzipinga na kutokuzipa kipaumbele karama za Roho Mtakatifu. 


Hivyo basi, kisingizio hicho cha wimbi kubwa la upotoshaji si sawa kabisa, na mtume Paulo hakuidharau wala kutokuipa kipaumbele karama hiyo, bali, alichokihubiri Paulo ni utaratibu wa utendaji kazi wa hii karama ya kenena kwa lunga kanisani ambapo aliisema…

1 Wakorinto 14:27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.

 28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.

Na tena alisema

 1 Wakorinto 14:13  Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri. 

Pia si  kwa utaratibu wa karama hiyo ya kunena kwa lugha tu, bali na hata karama ya unabii pia..

1 Wakorinto 14:29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. 

30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze. 


Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu

Ikiwa utakuwa na swali lolote kuhusu biblia, basi, wasiliana nasi kwa namba hizi

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.



MADA ZINGINEZO

NI KWA NAMNA GANI BWANA YESU ALIKUJA KUTIMILIZA TORATI NA MANABII?


Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)



HESHIMA YANGU IKO WAPI? 


TAFUTA PESA!  TAFUTA PESA! 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *