Ni mambo ya nyumba ipi ambayo mfalme Hezekia aliambiwa kuyatengeneza? (Isaya 38:1)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: ni mambo ya nyumba gani ambayo mfalme Hezekia aliambiwa ayatengeneze kwani atakufa? 

Isaya 38:1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO; MAANA UTAKUFA, wala hutapona. 

JIBU: Mambo ya nyumba ambayo mfalme Hezekia aliyoambiwa kuyatengeneza sio jengo la kifalme alilokuwa akiishi ndani yake, hapana! Bali ni mambo ya mwili wake wa damu na nyama, ambao siku zote unapinga kufanya mapenzi ya Mungu, hiyo ndiyo nyumba aliyoambiwa kuitengeneza, kwani mwili huu tulio nao ndio nyumba ya maskani yetu ya hapa duniani, maandiko yanasema hivyo katika..

2 Wakorinto 5:1 Kwa maana twajua ya kuwa NYUMBA ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.

2 Maana katika NYUMBA HII TWAUGUA, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 

3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.

 4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.

5 Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho.

6 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. 

Umeona hapo?…Na kauli hiyo ya Bwana kumtaka mfalme Hezekia kutengeneza mambo ya nyumba yake, yaani mwili wake, ilikuja baada ya mfalme Hezekia kumtemda Bwana dhambi (2 Nyakati 32:25).


Ndivyo ilivyo na sasa pia, wanadamu tunamtenda sana Bwana dhambi kwa rushwa zetu tunazotoa na kupokea, kwa uzinzi na uasherati tunaoufanya, kwa starehe na anasa tunazozipenda katika dunia hii, kwa uongo na maneno machafu katika vinywa vyetu, kwa uuaji, kwa ubakaji, kwa uchawi na uganga, kwa ibada za sanamu na wafu tunazozifanya, kwa kuwaonea yatima na wajane, kwa utazamaji wa picha chafu za ngono na ukahaba vichochoroni, kwa kupenda kuvaa nusu uchi na suruali kwa wanawake, kwa usengenyaji na kutokuwaheshimu wazazi wako, kwa mambo hayo na mengine mengi sana tumamkosea Bwana Muumbaji Wetu. Na kama ilivyokuwa kwa Mfalme Hezekia, Mungu anatupa onyo na taarifa na kwetu sisi pia kama alivyofanya kwa mfalme Hezekia, kuwa “TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO SASA MAANA UTAKUFA


Tengeneza mambo ya nyumba yako wewe mama/baba maana utakufa, tengeneza mambo ya nyumba yako wewe kaka/dada maana utakufa, tengeneza mambo ya nyumba yako wewe mzee/kijana maana utakufa, Mungu hajari cheo chako wala wadhifa wako, anachotaka yeye ni utengeneze mambo ya nyumba yako wewe Rais/waziri maana utakufa, wewe mfalme/malaika maana utakufa, anataka utengeneze mambo ya nyumba yako wewe askofu/mchungaji maana utakufa, tengeneza sasa mpendwa mambo ya nyumba yako kabla kifo hakijakufika ghafla, tengeneza kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa katika maji tele kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kama ulikuwa hujafanya hivyo, na hakika Bwana atakuokoa na shimo la uharibifu na kuzitupilia nyuma dhambi zako zote kama ilivyokuwa kwa mfalme Hezekia.

Isaya 38:17 Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; LAKINI KWA KUNIPENDA UMENIOKOA NA SHIMO LA UHARIBIFU; KWA MAANA UMEZITUPA DHAMBI ZANGU ZOTE NYUMA YAKO. 

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.


Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?


Unaweza kunitajia kanisa la kweli siku hizi za mwisho?


UMEPATA FAIDA GANI?


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)

LEAVE A COMMENT