Unaweza kunitajia kanisa la kweli siku hizi za mwisho?

  Kanisa, Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Je! Unaweza niambia na kunielekeza kanisani gani ni sahihi katika siku hizi za mwisho ili nikashiriki hapo? kwa sababu kila sehemu unapoenda ni manakisa yamejaa na kila mtu anahubiri habari za Yesu hadi mtu unachanganyikiwa na unashindwa kufahamu lipi ni sahihi na lipi ni la uongo.


JIBU: Kwanza fahamu kitu hiki, suala la watumishi wengi wa uongo kuongezeka sasa hivi ni kitu ambacho hatuwezi kukizuia, huo ni utimilizwaji wa maneno ya unabii aliyoyatoa Bwana Yesu Mwenyewe aliposema, manabii na makristo wengi wa uongo, yaani mitume wa uongo, manabii wa uongo, wainjilisti wa uongo, wachungaji na waalimu wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi.

Matayo 24:11  Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 

Soma tena

Marko 13:22  kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. 

Hivyo maneno hayo ya unabii ya Bwana Yesu hayana budi kutimia kama na mengine yalivyotimia na yatakavyokuja kutumia.

Lakini, ijapokuwa kuna hao watumishi wengi wa uongo, pia wapo na watumishi wengi wa ukweli wa Mungu, yaani mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Ukitaka kuelekezwa mtumishi gani wa Mungu wa kweli au kanisa la kweli ili uende utakauwa haujafanya vibaya endapo tu mtu huyo uliyemuuliza anamfahamu mtumishi wa Mungu wa ukweli, lakini je! Vipi endapo uliyemuuliza hajui au ni mtumishi wa shetani na ana lengo la kukupotosha? Maana watumishi wa uongo kazi yao ni kupotosha na si nyingine. Hivyo basi, hiyo tu haitoshi, unatakiwa wewe binafsi uwe na kitu cha ziada kitakachokufanya usipotezwa na kukusaidia wewe kujua kanisa linalohubiri kweli ni lipi, na kitu hicho sio kingine zaidi ya MAARIFA YA NENO LA MUNGU, ukiwa nayo hayo ndugu ndiyo yatakayo kupeleka sehemu sahihi na yatakusaidia kumtambua mtumishi wa kweli na wa uongo.


Ili tuelewe vizuri, hebu tafakari mfano huu; sasa hivi ukienda kwenye maduka ya simu, utakutana na simu nyingi sana ambazo ni feki, karibia kila maduka, simu feki ndizo zilizojaa, sasa hii haimaanishi kuwa, hakuna simu original, hapana! Simu original zipo na feki pia zipo. Lakini ukiwa na haja ya kununua simu original, huna budi kuwa na MAARIFA KUHUSU SIMU ORIGINAL, yaani ni lazima kufahamu simu original huwa ina sifa gani na nikiona vitu flani flani, ndipo nitathibitisha kuwa simu hii ni original. Lakini ikiwa huna hayo maarifa kuhusu simu original, utaenda dukani na utadanganywa na kuuziwa simu feki ambayo hukuitaka na huku nia yako ilikuwa ni upate simu original, sasa hivyo ndivyo ilivyo katika nyakati hizi za mwisho, kuna injili mbili zinazohubiriwa, feki na original, endapo wewe unataka injili original au kanisa original, huna budi kwanza kuwa na MAARIFA KUHUSU INJILI YA KWELI NI IPI NA INASEMAJE? Kisha hayo maarifa ndiyo yakupeleke sehemu sahihi, popote pale utakapoenda duniani,  kwa kutumia hayo maarifa ndipo utaweza kutambua kanisa sahihi. 


Maarifa haya nitayatolea wapi?

Maarifa hayo utayapata katika biblia yako takatifu, ukitaka kusikia sikia tu bila kusoma biblia yako ili kupata hayo maarifa ya Kristo na neno lake, hakika utapotezwa na mafundisho ya uongo. Hivyo unayo haja ya kurejea biblia yako ili ikuongoze sehemu sahihi.

Kumbuka: MAARIFA YA MUNGU SIO HILO DHEHEBU LAKO.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu

Bwana akubariki, shalom.

+255652274252/ +255789001312Mada zinginezo:

KANISA LA KWELI NI LIPI DUNIANI?


Kuna injili ngapi katika biblia?


Sabato zilizowekwa na wanadamu ni zipi? 

Je ubatizo sahihi ni kwa jina la Yesu au Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?


JINSI AMRI YA UPENDO INAVYOWAFANYA WATU WADUMU KATIKA DHAMBI


Je! Busu kanisani kwa watu wanaofunga ndoa ni sawa? 

LEAVE A COMMENT