MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 06)

  Siku za Mwisho, Uncategorized

Karibu tena kwa mara nyingine katika mfululizo wa makala hii fupi inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayopotosha watu wengi nyakati hizi za mwisho, tulishayatazama baadhi ya hayo makanisa na mafundisho yao potofu huko nyuma katika sehemu zilizopita, hivyo, ukiona mahali ulipo katika kanisa lako ni moja wapo ya hayo, huna budi kuchukua hatua ya kutoka katika kanisa hilo la uongo na kuachana na mafundisho yao, kwani biblia inasema…

2 Wakorinto 6:15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? 

Na tena inasema..

2 Wakorinto 6:17 Kwa hiyo, TOKENI KATI YAO, MKATENGWE NAO, ASEMA BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 

Toka kati ya hilo kanisa la uongo lililojaa mafundisho potofu yasiyokupa waokovu wa roho yako, ASEMA BWANA, na anza kumtafuta Mungu katika kweli ya neno lake kwa kurejea hiyo biblia yako, kwani Mungu Mwenyewe anawatafuta watu kama hao ili wamwabudu (Yohana 4:23). Chukua hatua hiyo mapema!Sehemu ya sita (06) karibu.

KANISA AMBALO MSINGI WAKE SIO BIBLIA TAKATIFU PEKEE.

Kanisa la Kristo msingi wake unapaswa kuwa ni maandiko takatifu tu pekee (biblia), na sio kitu kingine chochote, sasa unaweza uliza, hivi kuna kanisa ambalo msingi wake sio maandiko matakatifu tu peke yake? Jibu ni ndio, makanisa hayo yapo na tena ni mengi, na mfano wa hayo ni kanisa katoliki, ambalo msingi wa imani yake haujajengwa kwenye biblia takatifu peke yake bali na mapokeo mengine ya uongo ambayo yanapingana na biblia takatifu.


Nilishawahi muuliza mtu wa dhehebu hilo kama angeweza nithibitiashia kwenye maandiko matakatifu kuwa Mariamu ni kimbilio la wakosefu badala ya Yesu Kristo, au ni wapi biblia iliposema kuwa watu wenye dhambi wanapaswa kukimbilia kwa Mariamu na sio kwa Yesu Kristo? Jibu alilonipa lilinishangaza sana, alisema, “hivi unategemea kila kitu kiandikwe kwenye biblia?” 

Ndugu, mitume na manabii watakatifu wa Bwana hawakufundisha wala kuhubiri kitu chochote kile ambacho hakikutoka kwenye maandiko matakatifu, hata mtume Paulo alisema, sisemi kitu kingine chochote ila yale yaliyosemwa na Musa na manabii, (Matendo 26:22), hivyo, jiulize mara mbili mbili, msingi wa mapokeo ambayo yapo kinyume na maandiko matakatifu uliyopewa na kuaminishwa yametoka wapi kama si kwa ibilisi?

Mfano; utaambiwa Mariamu aliwatokea watoto Lusia, Francisco, na Yasinta huko Fatima, hivyo hatuna budi kumwomba Mariamu kwa kusali rozari kwa sababu tu kiongozi wako kasema Mariamu ni dira na mwongozo wa toba, ndugu umedanganywa, huo ni uongo, biblia haituagizi kuomba wala kusali kwa mwanadamu yoyote yule wala malaika bali ni kwa Mungu tu, na tena dira ya toba ni Kristo pekee, Mariamu hakufa kwa ajili dhambi ya mtu yoyote yule, ndoto au maono yoyote yanayopingana na biblia (kama hiyo ya watoto Fatima kuwa umuombe Mariamu), hayatoki kwa Mungu bali kwa ibilisi, kwani huyo pekee ndiye anayeweza kukuambia uombe kitu kingine tofauti na Mungu, hivyo toka katika hilo kanisa lenye misingi hiyo potofu ambayo mitume hawakuihubiri


Wengine watakwambia sisi tunaamini biblia na Haile Selassie, wengine watakwambia tunaamini biblia na nabii fulani na kumfuata huyo, wengine watakwambia tunamwamini buddah n.k, kisha utapewa maneno machache na mistari kadhaa ya kukufariji na wewe unalidhika kabisa, utaambiwa tuwe na umoja, tuwe na upendo, na kuaminishwa utaingia mbinguni kwa hivyo, na huku upo katika taasisi ya uongo ambayo ina msingi mwengine tofauti na biblia. Ndugu, tambua kuwa, hata kama ukiwa na upendo wa kuwasaidia walemavu wote duniani na huku hujamwamini Kristo na kubatizwa na kudumu katika fundisho la mitume huwezi ingia ufalme wa Mungu, biblia ipo wazi kabisa.

Watu hao wanaofundisha mambo ambayo hayakufundishwa na mitume wapo chini ya laana, hivyo jiokoe nafsi yako na laana hiyo kwa kutoka huko.

Wagalatia 1:8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. 

Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Koga ni nini katika biblia? 

Ni hukumu ipi ya Ibilisi inayozungumziwa katika Waraka wa (1 Timotheo 3:6?)


Je! Kuna Mungu wawili? (Kulingana na Yohana 1:1)


UFALME WA MUNGU NI NINI, ULITOKA WAPI NA ULIANZA LINI? (Sehemu ya 02)


Nini maana ya mstari huu “unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu” (2 Petro 2:21) 


UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?

LEAVE A COMMENT